MWIGIZAJI Bora wa Kiume Bongo, Jacob Steven ‘JB’ amefuatwa na mastaa Wazungu kutoka Ulaya nchini Norway.
Hivi karibuni, Ijumaa Wikienda lilimnasa JB akipigwa na baridi usiku
wa manane kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar
ambapo alipoulizwa kulikoni alisema kuna waigizaji kutoka Norway
wanaokuja kumfuata hivyo anawasubiri.
Alisema: “Kuna waigizaji
Wazungu kutoka Norway wanakuja kunifuata, nimekuwa nikiwasiliana nao kwa
muda mrefu, mwanzoni nilisita kwa kuwa nilikuwa siwajui. Baadaye
nilijiwa na mawazo kwamba kwa nini nisiwatafute mtandaoni? Kweli
nilipoingia mtandaoni na kutafuta majina yao niliwapata.
“Wapo
wawili, majina yao ni Bard Yuvis Akir na Vega Uvisakir, waliniambia
wanakuja kunichukua nikafanye nao kazi za filamu kwao, nikimaliza
Tamasha la Matumaini tutarekodi filamu moja hapa nchini ndiyo tuondoke.”
wakati mazungumzo yakiendelea, JB aliitwa kwenye mlango wa kutokea uwanja wa ndege na kuwapokea wageni wake kisha kutimua eneo hilo.
wakati mazungumzo yakiendelea, JB aliitwa kwenye mlango wa kutokea uwanja wa ndege na kuwapokea wageni wake kisha kutimua eneo hilo.
CREDIT:GLP
No comments:
Post a Comment