EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, July 29, 2013

MCHUNGAJI MBARONI KWA ULAWITI.


MCHUNGAJI wa kanisa moja la kilokole lililopo Kichangani, Majohe, Dar aliyetajwa kwa jina moja la Benard anadaiwa kutiwa mbaroni kwa tuhuma za ulawiti wa mtoto wa kiume (jina tunalo) mwenye umri wa miaka 15.
 
Hivi karibuni, gazeti hili lilipenyezewa kuwepo kwa sakata hilo ambapo lilitinga eneo la tukio na kuweka ‘patroo’ ili kunasa habari kamili.
 
Kwa mujibu wa mdogo wa mchungaji huyo aliyejitambulisha kwa jina la Hamis, kaka yake huyo alikamatwa wiki iliyopita baada ya watu waliojitambulisha kuwa ni askari kufika nyumbani na kumuweka chini ya ulinzi.
 
Alisema kuwa katika kuishi na kaka yake huyo, aliwahi kumuona huyo mtoto anayedaiwa kulawitiwa mara moja tu kwani yeye bado ni mgeni.
 
Kwa mujibu wa dogo aliyedaiwa kuingiliwa, alikutana na mchungaji huyo mwaka jana maeneo ya Stendi ya Banana-Ukonga, Dar ambapo alimuomba na kumwambia kuwa alikuwa anatafuta mtoto wa kumfanyia biashara ya mayai huko Majohe nyumbani kwake.
 
Alisema kuwa alikataa na kumwambia hawezi kwenda naye bali aende akazungumze na wazazi wake nyumbani.
 
Alisimulia kuwa baada ya hapo, aliongozana na baba mchungaji hadi kwa wazazi wake ambapo walikubaliana kuwa kila mwezi atamlipa mshahara wa shilingi 30,000.
Baada ya makubaliano hayo ‘dogo’ alisema kuwa aliondoka na mchungaji na baada ya kukaa kwa muda mfupi huku akiendelea na biashara ya mayai, mchunga kondoo huyo wa 
Mungu alianza tabia ya kumfanyia unyama huo huku akimdanganya kuwa atampa simu.
“Kuna wakati kweli ananipa simu kwa muda na kuninyang’anya.
“Kwa siku moja alikuwa ananiingilia mara mbili, asubuhi na jioni,” alisema mtoto huyo kwa uchungu.
 
Alisema kuwa baba mchungaji aliendelea kumfanyia ‘usodoma’ kwa muda mrefu.
Alisema baada ya kufika nyumbani kwa wazazi wake, mama yake alimgundua na kumtaka kueleza ukweli.
 
“Nilimweleza baba na mama jinsi mchungaji anavyonifanyia ukatili, walimwita nyumbani wakiwa tayari wameshaandaa polisi jamii, alipofika aliwekwa chini ya ulinzi lakini aliwaomba msamaha polisi jamii hao pamoja na wazazi huku akiahidi kutorudia tena.
 
“Kila mtu alikubaliana na msamaha na kumpa masharti kwamba afilisiwe vitu vyake vyote kama faini ya kosa.
 
“Alikubali, akafilisiwa vitu vyote  vikakabidhiwa kwa wazazi wangu ambapo baba yangu alikuwa mgonjwa hivyo kutokana na kukosa uwezo aliviuza vitu hivyo kwa ajili ya matibabu na mwishowe akafariki dunia,” alisema.
 
Mtoto huyo aliendelea kusimulia kuwa baada ya kuachana na mchungaji huyo kwa muda mrefu, kuna msichana mmoja mtaani kwao anayejulikana kwa jina la Asha ambaye alimfuata na kumbembeleza kuwa waende tena kwa mchungaji huyo, naye akakubali na baada ya kufika huko huku wakiwa wameambatana na mtoto mwingine wa kiume (17), mchungaji huyo alimfanyia tena mchezo huo na kumpa fedha huyo msichana hivyo akawa kama yeye ndiye aliyeenda kuwauza.
 
“Juzi hapa mtaani kwetu aliuawa mwizi mmoja, baada ya kuona kile kifo nilimuita mama yangu na kumwambia natubu maovu yangu ndipo nikaanza kumwelezea jinsi nilivyorudi tena kwa mchungaji kwa kushawishiwa na huyo Asha,” alisema mtoto huyo.
 
Huku mchungaji huyo akiwa na tuhuma hiyo ya kufanya mchezo huo na mmoja chumbani na mwingine sebuleni, mwanaume ambaye ni rafiki wa mchungaji huyo aliyetajwa kwa jina moja la Rahim naye akaingia kwenye mkumbo na kuendeleza dhambi ya kuwasulubu vijana hao.
 
Mchungaji huyo, rafiki yake na Asha, wote waliswekwa nyuma ya nondo za mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Stakishari, Dar na kufunguliwa shitaka namba STK/RB/13160/2013-ULAWITI wakisubiri kesi yao kuanza kuunguruma.
Wanahabari wetu walifanikiwa kuzungumza na askofu wa mchungaji huyo, Grace Joseph ambaye alikuwa na haya ya kusema:
 
“Kwa jinsi ninavyomjua mchungaji wangu siamini kama amefanya kitendo hicho hivyo tuhuma hizo sikubaliani nazo kabisa ila polisi wanaendelea na uchunguzi.”
Kwa upande wake mjumbe wa eneo la Kichangani, Majohe, Hawa Kidulu alieleza kuwa mchungaji huyo kweli alikamatwa na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo na mpaka sasa wahusika wameshikiliwa.
Via GLP

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate