MKONGWE kwenye soko la filamu Bongo, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ amesema
hatarajii kuolewa tena baada ya kuvunjika kwa ndoa zake ikiwemo ile ya
prodyuza, George Otieno ‘Tyson’.
Akisimulia maisha yake mbele ya paparazi wetu, Monalisa alisema kuna
siku walipokuwa kwenye kikao cha maandalizi ya send off ya mama yake
(Suzan Lewis ‘Natasha’), alitania kwa kusema ataolewa Desemba lakini
hakuwa ‘siriasi’.
“Sina mpango wa kuolewa kabisa, kwanza sina mchumba nitaolewaje? Siku ile nilikuwa natania tu kwa sasa sipo tayari kufanya tendo hilo,” alisema Monalisa.
“Sina mpango wa kuolewa kabisa, kwanza sina mchumba nitaolewaje? Siku ile nilikuwa natania tu kwa sasa sipo tayari kufanya tendo hilo,” alisema Monalisa.
Credit GLP
No comments:
Post a Comment