Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage jana alitoka nje ya Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oyesterbay chini ya ulinzi mkali baada ya kumalizika kwa mkutano wa klabu hiyo, ambao wanachama walishindwa kujadili kwa kina ajenda kutokana na vurugu na zomeazoea.
Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage jana alitoka nje ya Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oyesterbay chini ya ulinzi mkali baada ya kumalizika kwa mkutano wa klabu hiyo, ambao wanachama walishindwa kujadili kwa kina ajenda kutokana na vurugu na zomeazoea.
| Rage na Mzee Kinesi |
| Ibrahim Masoud Maestro na mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria Hans Pope |
Mwenyekiti Rage alijikuta kwenye wakati mgumu
kutokana na baadhi ya wanachama kumzomea wakati akiwasomea maelezo ya
mikakati na maendeleo ya klabu hiyo, ingawa mwishoni alifanikiwa
kuwatuliza baadhi ya waliompinga.
Kasheshe ya kuzomea-zomea iliendelea hata baada ya kuitwa mbele Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Tolly Mbwete kuzindua mpango mkakati wa maendeleo ya klabu hiyo.
Wakati Mbwete (Profesa) akisoma maelezo ya mkakati huo, baadhi ya mashabiki walisikika wakisema; “Hatutaki...hatutaki...toka, hatutaki kusikia habari ya Chuo Kikuu, tunataka matokeo mazuri uwanjani huo mkakati wenu hautusaidii.”
Pamoja na kuzomewa, Rage alimtaka Mbwete kuendelea kusoma maelezo ya mkakati huo huku kelele zikiongezeka kutoka kwa wanachama wengi, hali iliyowafanya wengine kushindwa kusikiliza kilichokuwa kikiongelewa.
Kama mwendelezo wa kupinga kilichokuwa kikiongelewa, baadhi ya wanachama waliondoka kwenye mkutano huo uliokuwa chini ya ulinzi wa askari zaidi ya 70.
Baada ya mambo kwenda vibaya, Rage aliwataka
polisi kuwakamata wanachama waliokuwa wakifanya fujo ikiwa ni pamoja na
kuwatishia kuwafuta uwanachama, jambo lililoibua zogo zaidi.
“Hatoki mtu hapa...tupo tayari kufa lakini hapa hatoki mtu...unatuburuza, hatukutaki...tumekuchoka ondoka,” wanachama walipaza sauti.
Mkutano huo, uliofunguliwa saa 3 asubuhi na kuhudhuriwa na wanachama 712 kati ya 1516 ambao ni hai, na wanachama hao walishindwa kuchangia kikamilifu ajenda hali iliyopelekea mambo mengi kupitishwa kienyeji.
Kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Simba ilipata kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya URA kutoka Uganda.
Simba walikuwa wa kwanza kufunga bao katika dakika
ya saba likifungwa na Betram Mombeki. URA walisawazisha kupitia kwa
Lutimba Yayo dakika 60, na kisha akafunga bao la ushindi dakika ya 76.
No comments:
Post a Comment