Akizungumzia
na mtandao huu, Bi Hindu alisema: "Yule bwana Rage jana katupeleka peleka
tu, badala ya kutuambia vitu vya msingi analeta porojo, ukimuuliza eti
katiba inampa mamlaka. Katuletea polisi ili atutishe, polisi apeleke
kwenye siasa za chama chetu CCM na sio kwenye Simba yetu. Sikupenda hata
ule mpangilio wa maswali, watu wenye hoja nzito alikuwa akiwakataa na
kuchagua wa kwake aliowapanga," alisema Bi Hindu.
Muigizaji mkongwe na mwanachama wa klabu ya Simba, Bi Hindu amesema hajaridhishwa kabisa na uendeshaji wa mkutano mkuu wa Simba uliongozwa na mwenyekiti Aden Rage.
No comments:
Post a Comment