Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ametoa somo la gesi na kuwataka wananchi wa Mtwara kuacha kujenga mtazamo kwamba nishati hiyo ni yao, kwani inapatikana ni kilomita 80 kutoka nchi kavu na kwamba kuichimba ni gharama kubwa.

Profesa Muhongo ambaye jana alikuwa akitoa somo kwa wananchi na wadau mbalimbali wa nishati na kusikiliza maoni yao kuhusu umuhimu wa nishati, alisema watu wamekuwa wakipiga kelele kisiasa badala ya kuzungumzia suala la gesi kitaalamu, ndiyo maana matatizo yanaendelea kuwapo.
“Ukifika hapo uingie kilomita mbili ukute ardhi ya bahari ndiyo uchimbe kilomita tatu kukuta gesi halafu wanasema ni yao.Mnatuelezaje gesi ni yenu kwa hali hiyo, hayo wanayozungumza ni masuala ya ajabu kabisa.”
Alisema ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka
Mtwara hadi Dar es Salaam umbali wa kilomita 534, linaendelea kujengwa
na litakamilika mwakani.
“Bomba hili siyo la Wachina kama inavyosemwa,
tumepata mkopo kutoka kwao wa Dola 1.2 bilioni za Marekani na ujenzi
wake utakamilika baada ya miezi 18,” alisema. Katibu Mkuu wa wizara
hiyo, Eliakimu Maswi, aliwataka wananchi wa Mtwara kuacha kulalamika na
kuzungumza mambo ya historia, bali wajitume kujiletea maendeleo.
“Tuache kulalamika kila siku na kuzungumza mambo ya historia, mtu mvivu ndiye mlalamikaji,” alisema Maswi.
No comments:
Post a Comment