WAKATI hali ya mmiliki wa maduka ya Home Shopping Centre, aliyemwagiwa
tindikali na mtu asiyejulikana, Said Mohammed Saad, ikiendelea kuimarika
kutokana na matibabu anayopata, hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa kutokana
na tukio hilo.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema polisi wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo.
“Jamani mambo mengine ni ya ndani ya polisi na si vema tukayatoa hadharani, tulieni jamani, upelelezi ukikamilika tutawaita na kutoa taarifa,” alisema Kamanda Wambura.
Saad alimwagiwa tindikali hivi karibuni maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam na mtu asiyejulikana.
Baada ya tukio hilo, mtu huyo ambaye hadi sasa hajakamatwa, alikimbia na kutokomea kusikojulikana.
Taarifa za kipolisi zilieleza kwamba, Saad alimwagiwa tindikali akiwa anazungumza na mfanyakazi wa duka lake lililopo kwenye Jengo la Msasani City Mall.
Tukio la kumwagiwa tindikali mfanyabiashara huyo, limekuja ikiwa ni wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba, ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa majimaji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali.

CHANZO NI GAZETI LA MTANZANIA
No comments:
Post a Comment