TAMASHA
la Usiku wa Matumaini linalotarajiwa kutimua vumbi Jumapili ya wiki hii
(Julai 7, 2013) ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ndiyo
habari ya mjini kwa sasa ambapo mashabiki watakaohudhuria watapata fursa
ya kushuhudia mseto wa burudani zenye uzani mkubwa, Showbiz
inakuchanganulia.
Burudani zitakuwa nyingi lakini baadhi ni mechi kali kati ya wabunge wa Simba watakaokipiga dhidi ya wale wa Yanga sambamba na wasanii wa Bongo Movie watakaooneshana kazi na wenzao wa Bongo Fleva, mwamuzi akiwa ni dakika tisini.
WABUNGE SIMBA VS YANGA
Mechi inayotarajiwa kuwa kivutio kikubwa kama ilivyokuwa mwaka jana, ni kati ya waheshimiwa wabunge wanaoshabikia timu mbili za Simba na Yanga ambao watachuana kumtafuta Bingwa wa Kombe la Matumaini 2013.
Ikumbukwe kuwa mechi kama hiyo, ilipigwa mwaka jana Uwanja wa Taifa ambapo Wabunge wa Simba waliibuka kidedea kwa kuwalaza Yanga kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
“Tumewaongeza kikosini Mrisho Ngassa, Ally Mustapha ‘Barthez’, Kelvin Yondani na Athuman Idd ‘Chuji’ ili kufuta uteja wa mwaka jana. Tutacheza kwa nguvu kuhakikisha Yanga inaibuka na ushindi. Hatuna utani katika mechi, sisi tunakwenda kulinda heshima,” alisema Mhe. Abbas Mtemvu, kiongozi wa kambi ya wabunge wa Yanga.
Kwa upande wa wabunge wa Simba chini ya kiongozi wao, Amos makalla, wamesema wanajiwinda kwa nguvu kuhakikisha Yanga hawatoki siku hiyo Taifa.
“Mpaka sasa tumeshawaongeza Shomari Kapombe na Amri Kiemba, tunatarajia kuongeza wengine baada ya kocha wetu kutoa mwongozo. Siku hiyo watake wasitake, tutawapiga tu, hawana ujanja. Mwaka huu tutawatengeneza ndani ya dakika 90,” alisema Makalla.
BONGO MOVIE VS BONGO FLEVA
Wasanii wa tasnia kubwa mbili, filamu na muziki wa kizazi kipya nao wataoneshana kazi siku hiyo huku dakika tisini zikiachwa ziamue nani mkali wa soka kati yao. Mwaka jana katika Tamasha la Usiku wa Matumaini, Bongo Movie walishinda bao 1-0, kwa hiyo mwaka huu Bongo Fleva wanataka kurejesha heshima yao.
“Tutawafunga kwa urahisi sana mwaka huu. Hatutaki kurejea makosa ya mwaka jana. Hili naomba hao Bongo Movie walijue. Mimi binafsi lazima niwafunge, nina usongo nao sana wale jamaa,” alisema Hamis Ramadhan ‘H. Baba’, nahodha wa Bongo Fleva.
Naye Mwenyekiti wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ alifunguka: “Kombe ni letu, Bongo Fleva wataendelea kuwa wateja wetu tu. Tunaendelea kufanya mazoezi makali, tupo vizuri sana. Mwaka huu tutawafunga zaidi ya mabao mawili.”
Kwa mujibu wa mratibu wa ishu hiyo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, pia kutakuwa na mechi ya kombaini ya wanafunzi wa shule za Makongo na Jitegemee ambao watafuana vikali kumtafuta mshindi.
Kama hiyo haitoshi, Mrisho aliongeza kuwa pia kutakuwa na mapambano ya ndondi ambapo wabunge Halima Mdee, Zitto Kabwe na Ester Bulaya watazichapa na wasanii wa filamu; Jacqueline Wolper, Ray na Aunt Ezekiel huku wakali wa ndonga kutoka Tanzania, Thomas Mashali na Francis Miyeyusho wakikalishana na wenzao kutoka Kenya, Patrick Amote na Shadrack Muchanje kuwania Ngao ya Amani ya Afrika Mashariki.
Pia kutakuwa na burudani ya muziki kutoka kwa wakali kibao kama tangazo (Uk. wa 8) linavyoeleza.
Hii siyo ya kukosa!!!

No comments:
Post a Comment