Wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri
Mohammed Morsi wamepanga maandamano zaidi kuelekea kambi za kijeshi.
Pia wameitisha maandamano makubwa hapo kesho Jumanne.
Haya yanajiri huku, Mjumbe wa mambo ya nje wa
Muungano wa Ulaya akiwa mjini Cairo kwa mazungumzo ya kumaliza taharuki
zinazoendelea kufuatia mauaji ya zaidi ya waandamanji 70 wengi wakiwa
wafuasi wa Muslim Brothehood .
Maelfu ya wafuasi wa Mohammed Morsi
wameendelea kupiga kambi nje ya msikiti mashariki mwa Cairo kwa majuma
kadhaa sasa na wanapanga kuendelea na maandamano yao usiku kucha.
Waandamanji hao wameitisha maandamano makubwa hapo kesho jumanne kuelekea katika kambi kuu ya jeshi.
Wanajeshi waliomuondoa madarakani Bw. Morsi wameonya waandamanaji dhidi ya kuhatarisha usalama wa kitaifa.
Wanajeshi wamesema yeyote atakayekiuka amri
atakabiliwa vilivyo.Tayari viongozi wengi wa Muslim Brotherhood
wamekamatwa au wamewekewa vibali vya kukamatwa.
Huku haya yakiarifiwa Mjumbe wa muungano wa
Ulaya Chatherene Ashton anakutana na pande zote za kisiasa nchini Misri.
Hata hivyo hali ya sasa ni dhahiri kwamba hakuna ushawishi wowote wa
kimataifa utakaobadilisha mzozo wa sasa.
No comments:
Post a Comment