Harakati ya Ikhwaanul Muslimiin ya Misri imetangaza kuwa, kwa
akali watu 480 wameuawa, 8,000 kujeruhiwa na wengine 1,500 kutiwa
mbaroni kwenye ghasia na machafuko yaliyodumu kwa wiki tatu nchini humo.
Chama cha Uadilifu na Uhuru, tawi la kisiasa la Ikhwaanul Muslimiin,
kimeeleza kuwa katika kipindi cha wiki tatu zilizopita, watu wasiopungua
mia nne na themanini wameuawa na wengine elfu nane kujeruhiwa pamoja
na kufungwa kanali tisa za televisheni za harakati hiyo.
Taarifa
zinasema kuwa, machafuko na mapigano nchini humo yamesababishwa na hatua
ya jeshi ya kumuondoa madarakani na kumuweka kizuizini Rais Mohammad
Morsi wa nchi hiyo.
Wafuasi wa Morsi wamekuwa wakijitokeza barabarani
kila siku kumuunga mkono kiongozi huyo na hivyo kukabiliwa na hatua kali
za jeshi.
Chanzo: kiswahili.irib.ir
No comments:
Post a Comment