Habari na Mahmoud Zubeiry.
AZAM
FC leo inatarajiwa kushuka dimbani kwenye Uwanja wa Soccer City,
unaojulikana pia kama FNB uliopo Soweto, Johannesburg, Afrika Kusini,
kumenyana na wenyeji, Kaizer Chiefs katika mchezo wa kwanza kwenye zaira
yake ya kujiandaa na msimu nchini humo.
Azam
iliyoondoka nchini jana mchana kwa ndege ya Shirika la Afrika Kusini,
kwenda Johannesburg, Afrika Kusini kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa
na msimu mpya, leo itaanza kazi kwenye Uwanja huo wenye uwezo wa
kuchukua mashabiki 94,736.
Timu
hiyo yenye maskani yake, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam,
iliyoondoka na kikosi chake kizima, kasoro wachezaji wawili tu majeruhi,
kiungo Mkenya, Humphrey Mieno na mshambuliaji Mganda, Brian Umony,
imefikia katika hoteli ya Randburg Towers.
RATIBA YA MECHI ZA AZAM AFRIKA KUSINI:
AGOSTI 5, 2013:
Azam Vs Kaizer Chiefs
AGOSTI 7, 2013:
Azam Vs Mamelodi Sundwons
AGOSTI 9, 2013:
Azam Vs Orlando Pirates
AGOSTI 12, 2013:
Azam Vs Moroka Swallows
Azam
jana ilifanya mazoezi yake ya kwanza kwenye Uwanja wa Wits University
asubuhi na jioni na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall
amefurahishwa na mazingira ya kambi na Uwanja wa mazoezi.
“Tumepata
mazingira mazuri ya kambi, Uwanja wa mazoezi na mechi nzuri za kujipima
nguvu. Vijana watanufaika sana na kambi hii na itakuwa sababu ya
kufanya vizuri katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, tukianza na
kuchukua Ngao,”alisema.
Baada
ya mchezo wa leo, Azam itashuka tena dimbani Agosti 7, kumenyana na
Mamelodi Sundowns kabla ya kuivaa Orlando Pirates Agosti 9 na Agosti 12
itamaliza ziara yake kwa kumenyana na Moroka Swallows.
Azam
inatarajiwa kurejea nchini Agosti 13 tayari kwa mchezo wa kuwania Ngao
ya Jamii kuashiria kufungua pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC, Agosti 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Safari
hii Azam, washindi wa pili mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu wamepania
kutwaa Ngao mbele ya Yanga, baada ya mwaka jana kufungwa na Simba SC na
kocha Muingereza Stewart Hall anajiandaa kikamilifu kwa ajili hiyo.
No comments:
Post a Comment