
Michael Richard Wambura.
YAH: SABABU ZA KUUNGA MKONO
UAMUZI WA MSAJILI WA VYAMA VYA MICHEZO NA VILABU KUKATAA KUSAJILI
MAREKEBISHO YA KATIBA YA TFF KUTOKANA UKIUKWAJI WA UTARATIBU NA
SHERIA ZA MAREKEBISHO YA KATIBA TFF 2013
Katiba ya TFF ya 2012 ilifutwa na msajIli wa vyama vya
michezo na vilabu kwa kuwa ilibadilishwa kinyume cha sheria (BMT)
pamoja na Katiba ya TFF ibara ya 30 kwa kutumia njia ya waraka badala
ya Mkutano Mkuu, hivyo katiba halali kisheria inayotambulika ni ile ya
2006 na mabadiliko yake .
FIFA na Serekali kupitia wizara yenye dhamana
na michezo iliiagiza TFF iitishe Mkutano Mkuu ili ifanye mabadiliko
ya katiba stahiki kwa mujibu wa katiba na kwa kufuata taratibu
zilivyoainishwa kwenye katiba ya TFF. Nimelazimika kuendelea kuiunga
mkono Serikali kupitia msajili kwa maamuzi yake ya kukataa kusajili
mabadiliko ya katiba ya TFF kwa kuwa TFF kwa makusudi imeendelea
kuvunja katiba yake katika kufanya mabadiliko.
Kisheria msajili husajili mabadiliko yoyote ya Chama kilichosajiliwa chini ya Sheria ya BMT kwa kuzingatia Sheria NA 12 ya 1967 na marekebisho yake NA 6 ya 1971 ya Baraza la Taifa la Michezo pamoja na Kanuni za Baraza la Michezo la Taifa na Kanuni za Usajili NA 422 za1999.
Chama chochote kitakacho kwenda kinyume na sheria hizo
hikiwezi kupewa usajili au Katiba yake na marekebisho yake hayawezi
kupewa usajili,aidha uamuzi wa msajili sio tu utaifanya TFF peke yake
itambue sheria bali hata vyama vingine vitawajibika kufuata utaratibu
katika kufanya mabadiliko ya katiba zao,
Katiba ni nyaraka ya kisheria hivyo chombo chenye
mamlaka kisheria hapa Tanzania ya kutafsiri katiba ni Mahakama pale
pande mbili zinapotofautiana juu ya tafssiri ya Katiba, hivyo kwa
kufanya hivyo msajili atakuwa ameepusha suala la Katiba ya TFF kuingia
katika mikono ya kimahakama kwa kuwa utaratibu uliotumika kubadili
katiba ya TFF ni dhahiri haukufuata taratibu zilizoainishwa kwenye
katiba ya TFF na sheria na za nchi kama zilivyoaanishwa. Sababu kuu
zinazonipelekea mimi kuunga mkono uamuzi huo ni kama zifuatazo:
- 1. UPIGAJI KURA MAREKEBISHO YA KTIBA
Ibara ya 30(4) ya katiba ya TFF 2006 inaelekeza ya
kuwa mapendekezo ya mabadiliko ya katiba ya yatapitishwa ikiwa
yataridhiwa na wajumbe theluthi mbili(2/3) ya wajumbe wenye haki ya
kupiga kura.
- Ibara ya 28(4) maamuzi yote ya mkutano mkuu yatafanywa kwa kuzingatia uwingi wa kura halali zitakazopigwa na wajumbe halali wa Mkutano Mkuu labda ikiwa katiba ya TFF inaelekeza vinginevyo. “ Unless otherwise stipulated in the statutes the decisions of the general assembly shall be taken by simple majority of the votes validly cast by the official delegates”.
- Ibara 28(5) ya katiba ya TFF(MAAMUZ)
Inazungumzia Maamuzi yanayohusiana na mabadiliko yoyote ya makao makuu ya TFF, mabadiliko yoyote ya Katiba na Kanuni zake,
marekebisho yoyote ya ajenda kwenye mkutano mkuu wa kawaida, maamuz
iyoyote yanayohusiana na kusimamishwa au kufukuzwa mjumbe wa vyombo vya
TFF au inayohusiana na kuvuliwa hadhi ya Urais wa heshima au
mwanachama wa TFF au inayohusiana na kutengwa kwa mwanachama au
kuvunjika kwa TFF lazima itahitaji zaidi ya 2/3 ya kura halali zililizopigwa na wajumbe resmi wa Mkutano Mku “
Decision relating to any change of head office of TFF ,any amendments
of Statutes and regulations, any modification to the agenda of the
ordinary general assembly, any decision relating to suspension or
dismissal of member a member of an organ of TFF or relating to
bestowing of the title of honorary president or member of the TFF or
relating to the exclusion of a member of TFF or dissolution of TFF shall
require a majority of 2/3 of the votes validly cast by the official
delegates”.
Kwa kuwa hakuna kura zilizopigwa na wajumbe wa mkutano
mkuu wa TFF na kuhesabiwa kuamua ama kupitisha au kukataa mabadiliko
basi zoezi hilo na marekebisho hayo ni batili kwa mujibu wa Katiba ya
TFF.
- 2. MKUTANO MKUU WA DHARURA
Ibara ya 25(4) katiba ya TFF ya 2006 inaelekeza kuwa
Agenda na makabrasha ya Mkutano Mkuu ni lazima yawafikie wajumbe wa
mkutano mkuu walau siku 15 kabla ya mkutano Mkuu.
Kwa kuwa wajumbe walipewa agenda na makabrasha siku
moja kabla ya Mkutano Mkuu, huo ulikuwa uvunjaji mkubwa wa Katiba ya
TFF , wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF hawajiwakilishi wao bali wana
wakilisha Mikoa, Vyama shirikishi na Vilabu ambavyo vina wanachama
wake na kamati zake za utendaji ambazo zilikuwa na haki ya kujadili na
kuwapa wawakilishi wao mawazo yao kwani maamuzi ya ya TFF yanagusa
kuanzia ngazi ya Taifa mpaka wilaya.
- 3. KUINGIZA VIFUNGU KWENYE KATIBA BILA KUJADILIWA NA KUPITISHWA NA MKUTNO MKUU WA TFF
Kwa kuwa marekebisho ya katiba kwa kutumia waraka ya
2012 yaliyowasilishwa kwa msajili, usajili wake ulifutwa hiyo
maraekebisho yote yaliyofanyika wakati huo ikiwa ni pamoja ibara Ibara
52 (1(b),2,3,4,5,6(a,b) yanayohusu Kamati ya Uchaguzi na kamati ya
Rufaa ya Uchaguzi iliyopelekea Uteuzi wa Mtinginjola na kamati yake ,
pamoja na Ibara ya 64(1,2) ya leseni za vilabu yanakuwa batili,
hivyo kama TFF ilikuwa bado inapenda vifungu hivyo viwemo kwenye
marekebesho ya katiba ya 2013, basi njia sahihi ilikuwa ni kuwasilisha
maombi kwenye mkutano Mkuu wa TFF 13/7/2013 kwa mujibu wa Katiba ya TFF
ibara 30 (2006).
Kwakuwa TFF haikupeleka maombi ya mabadiliko haya na
kupitishwa na Mkutano Mkuu wa TFF 2013 hivyo kuyaingiza kwenye katiba
ya sasa ya 2013 na kuyaombea usajili kwa msajili ni kinyume na sheria
na Katiba ya TFF, tafsiri rahisi ni kuwa TFF ilitaka kuonyesha kwa
Umma wa Watanzania ya kuwa serekali kupita msajili wa vyama vya michezo
haikuifuta na haikuwa na mamlaka ya kuifuta katiba ya Tff na
mabadiliko yake ya Desemba 2012.
- UUNDWAJI WA KAMATI KABLA YA MAREKEBISHO YA KATIBA KUSAJILIWA.
TFF iliamua kuunda kamati zake hata kabla katiba
haijasajiliwa na Msajili wa vyama vya michezo na vilabu, hii naonyesha
jinsi ambavyo mfumo mbovu ulivyozoeleka huko nyuma ambapo msajili
alikuwa akisajili katiba bila kuzingatia mapungufu hivyo kufanya vyama
vya michezo kuwa kama mali za watu binafsi na hata wakati mwingine
kumuona msajili kama sehemu ya vyama vyao jambo ambalo Wizara imeamua
kulifuta na kuhakikisha taratibu zinafuatwa.
Kwa mujibu wa katiba ya TFF ibara ya37(3)i (2006) Rais
wa TFF anayo mamalaka ya kupendekeza kwa kamati ya Utendaji majina ya
wajumbe wa vyombo vya TFF(TFF Organs) zilizoko kwenye katiba ya TFF
ibara ya 44(a,b)(kamati ya nidhamu na Rufaa),ibara 48(mahakama ya
usuluhishi,49(Kamati ya Uchaguzi), pamoja na kamati ndogo ndogo
(standing Committees) zilizoainishwa kwenye Ibara ya 39(1)a-i,
isipokuwa hana mamlaka ya kuteua wajumbe wa kamati za vyombo ya
TFFambavyo havimo kwenye katiba ya TFF (2006) kama kamati ya Rufaa ya
Uchaguzi, kamati ya Maadili na Kamati ya Rufaa ya Maadili.
Uteuzi wa Majaji na Wanasheria waandaamizi kuingia
kuongoza kamati ambazo zina utatata wa kisheria kumeidhalilisha sana
idara ya Mahakama na wanasheria kwa Ujumla hali ambayo huenda kwa siku
za usoni Majaji / Mahakimu na wanasheria waandamizi hawataweza kukubali
kushirikiana tena na TFF.
Hata hivyo uundwaji wa kamati hizi ni
dhahiri ulikuwa ni wa hila kwa kuwateua majaji ili ionekana haki
ingetendeka huku TFF ikijua wazi maamuzi yao kwa mujibu wa katiba
yanazingatia upigaji wa kura zaidi pale pande mbili zinapopingana kwani
ukiachila majaji kwenye kamati hizi wajumbe wanaobaki ni wale wale
ambao kwa mtindo wa Kura wanakuwa wengi(wengi wape)
TFF inaelekeza kuwasilisha malalamiko ya uchaguzi
kwenye vyombo vyake ambavyo ndio hivyo vilivyo haribu mchakato wa
Uchaguzi ambao hadi sas haujafanyika.Katika kuonyesha dhamira isiyo
nzuri ya kutaka kuwa na uchaguzi usiokuwa huru na wa haki TFF imewateua
na kuwabadilisha wajumbe ambao kwa sehemu kubwa walishiriki kuharibu
mchakato wa uchaguzi uliopita kwa kuwapa majukumu ambayo kwa njia moja
au nyingine bado watashiriki katika mchakato wa uchaguzi unatarajia
kufanyika siku za hivi karibuni, mfano ni wajumbe 3 kati ya 5 waliokuwa
kwenye kamati ya Rufaa ya chaguzi ya TFF wamehamishiwa kwenye Kamati
ya Maadili ya TFF(Francis KebweMohamed Mpinga,madundo Mtambo na mmoja(
Murtaza Mangungu Kamati ya
Rufaa ya Maadili,aidha wajumbe 4 wa kamati
ya Uchaguzi Kati ya 5 wamebakishwa kwenye kamati ilie ile na wawili kati
yao wamepandishwa vyeo na kuwa mwenyekiti na Makamu wa Kamati hizo
ambao Hamidu Mbwezeleni (mwenyekiti), Moses Kaluwa (m/mwenyekiti),
Hassan Dyamwale na Kitwana Manara. Katika
shauri lilifunguliwa mahakama kuu M.A. Ndolanga & others v National Sports Council and Other
[HCT, 1996, TLR 325,Bubeshi,J.] lililohusu uchaguzi mkuu wa FAT
ambalo maamuzi yake hayajawahi kutenguliwa na mahakama nyingine ya juu
nchini mpaka sasa, matatizo kama haya yalijitokeza na ambapo mahakama
pamoja na hoja nyingine ilitaka kujua:)
(i) Kama Kamati ya Usaili ya
uchaguzi ya BMT iliundwa kwa kufuata misingi ya
sheria?
(ii) Kama kamati ya usaili ya Uchaguzi ya BMT
ilifanya kazi kwa kuzingatia haki
asili za kimsingi (Natural Justice and Fair Play)
UAMUZI WA MAHAKAMA ULIMPA USHINDI M.A. NDOLAGA
Mahakama iliamua kuwa Vyombo vya maamuzi vya kiutawala wakati wa
kutekeleza majukumu yake ambayo yanahitaji kutambuliwa kisheria,
vinawajbu wa kutenda kwa kufuata sheria kwa kuzingatia haki za msingi
ikwa na maana ya kufuata utaratibu ambao msingi wake utahitaji Uhuru nje
ya maslahi na upendeleo kutoka upande wa chombo cha maamuzi kiutawala
na haki ya uwazi ya kusikilizwa kwa wale ambao wataathiriwa moja kwa
moja na maamuzi. “it is trite to remark that an administrative
body exercising functions that impinge directly on legal recognized
interests, owes it as a duty to act judicially in accordance with the
rule of natural justice which basically means the adoption of
procedure, which fundamentally demand freedom from interest and bias on
the part of the administrative body and the right to fair hearing for
those who are immediately affected by its decision”(pg 333)
Kwa kuwa uundwaji na malengo ya kamati hizi zina
walakini kisheria ni wazi uwezekano wa wadau kutafuta msaada wa kisheria
mahakamani unaweza kujitokeza kwa kzingatia ukiukwaji mkubwa wa haki za
msingi (Natural Justice) na Katiba ya TFF inavyoelekeza
- 5. UKOMO WA MADARAKA WA VIONGOZI WA VYAMA
TFF imehusishwa sana na hila na nia ya kuvuruga uchaguzi
ili waandelee kuliongoza shirikisho kinyume na katibaTFF Ibara ya 33
ya katiba ya tff inazungumzia Ukomo wa madaraka ni miaka 4 na uongozi
wao ulikoma Desemba 2012 hivyo uongozi huu kuendelea kuwepo madarakani
na kufanya marekebisho ya katiba ni kinyume na katiba ya TFF na sheria ya BMT ibara 15(1)a. “chama cha mchezo wowote kilichojishirikisha na BMT kitakuwa na wajibu wa kufanya kazi zote za chama kwa msingi wa katiba yake”
kwa mujibu wa Katiba ya na kanuni za usajili wa vyama vya michezo
kisheria isinge kuwa halali kw a msajili kusajili marekebisho ya Katiba
ya TFF kwa kuwa yanapingana na sheria za BMT na Msajili
kifungu7(1,2,3,4&5). Vinavyo someka kama ifuatavyo:
- 7(1). “Kipindi cha Uongozi wa Chama chochote kitamalizika mara kipindi cha kufanya uchaguzi mwingine kitakapokuwa kimefika kwa mujibu wa katiba ya chama “ ambapo TFFilikuwa Dec 2012
- 7(3) “Viongozi wanaomaliza muda wao watatakiwa waitisha mkutano mkuu wa Uchaguzi katika Kipindi ha siku 30 kabla ya siku ya ya mwisho ya kipindi cha Uongozi” Jambo ambalo TFF haikulifanya kwa makusudi kwa kingizio cha kupisha mabadiliko ya katiba kwa njia ya waraka ambayo ni kinuyume cha Katiba Ya TFF.
- 7(4). “Endapo siku 30 zitamalizika baada ya kipindi cha uongozi kumalizika bila ya uchaguzi kufanyika ,na bila ridhaa ya wanachama wa chama husika, viongozi wanaomaliza muda wao watahesabika kuwa wamejivua Uongozi” kwa kuwa Uongozi wa TFF haujapata ridhaa ya kuendelea kuongoza TFF kutoka kwa wanachama wake. kisheria hawakuwa na mamalaka ya kufanya na kusimamia mabadiliko ya katiba hivyo msajili kuyakataa ni utekelezaji wa sheria za nchi.
- 7(5). “ Endapo Viongozi wanaomaliza muda wao wamepata ridhaa ya wanachama kuendelea kuongoza baada ya kipindi cha uongozi kumalizika, wanaweza kukiongoza chama husika kwa kipindi kisicho siku 90 tu baada ya siku ya mwisho ya kipindi cha uongozi. Hata hivyo, ridhaa ya wanachama lazima iwe imepatikana kabla yatarehe ya mwisho ya kipindi cha Uongozi”.
Kwa mantiki hii Kamati ya Utendaji ilimalizi muda wake
14/12/2012 na haijaahi kupatiwa ridhaa na wanachama wake na hata kama
ingepata ridhaa, ridhaa hiyo ilikuwa na ukomo mwezi wa March 2013 ,
hivyo kamati hii haikuwapo kihalali wakati wa mchakato wa kubadilisha
katiba na hivyo kwenda kinyume kanuni za Usajili wa vyama vya michezo 11(1)d “ mabadiliko hayo hayafai kwa kuwa hayakuzingatia Sera ya Michezo ,Sera ya Utamaduni na sheria ya Baraza la Michezo”
- 6. HILA ZA KUVURUGA MCHAKATO WA UCHAGUZI
TFF imejiongezea muda wa kukaa madarakani zaidi ya
Miezi 7 sio kwa sababu yoyote ya msingi zaidi ya mikakati yenye hila ya
kuwaondoa wagombea wasiowahitaji tangu wakati wa kurekebisha katiba kwa
njia za hila za waraka ili kuunda kamati zitakazo tekeleza malengo yao
na hadi sasa wanaendelea na mkakati huo ili kuidhalilisha serekali
kwa kuwa ilionyesha msimomo wake wa kutaka wagombea watendewe haki,
swali ni vipi watu walioharibu mchakato wa uchaguzi uliolalamikiwa na
Wadau na serekeli wapandishwe vyeo tena washiriki katika mchakato huo
huo wa uchaguzi na ni vipi watu ambao hawakuwatendea haki wagombea kwa
kuwakata na kuwaondoa kwenye mchakato kwa hila mara ya kwanza watatenda
haki tena. Hii ni kinyume na sheria za BMT na kanuni za msajili Kifugu
11(3)b.kwa kuwa nia ya TFF ni kuwanufaisha wachache
Kwa kuwa Marekebisho ya Katiba ya Tff hayakuzingatia
katiba ya TFF na sheria za BMT na Kanuni za Msajili wa Vyama ninaunga
mkono uamuzi wa Msajili kukataa kusajili mabadiliko haya kwa
kuzingatia kanuni za msajili kama ifuatavyo:
- 11(3)a, Mabadiliko hayo yanaweza kuhatarisha usalama na kuvuruga amani miongoni mwa wanachama na jamii kwa ujumla na hivyo kuathiri maeneleo ya chama”.
- 11(1)b, Mabadiliko hayo yanalenga kuwanufaisha wachache”.
- 11(1)d, mabadiliko hayo hayafai kwa kuwa hayakuzingatia Sera ya Michezo ,Sera ya Utamaduni na sheria ya Baraza la Michezo.
USHAURI:
1.Kwa Kamati ya Utendaji chini ya L.C Tenga
imemaliza muda wake kisheria na imeshindwa kwa mara nyingine kuandaa
katiba ili kuipeleka TFF katiak Uchaguzi ambao utakuwa wa haki na huri
ni vizuri na busara inaelekeza kwa Bwn Tenga na kamati yake kawajibika
kwa kujiuzulu ili kupisha uundwaji wa kamati ya mpito (normalization
Committee) kama ilivyofanyika nchi za Sieraleon, Gambia, Cameroon na
Tanzania(2001)ili kuandaa njia huru kuelekea uchaguzi mkuu kupata
viongozi wapya.
2. Kwa kuwa Uongozi uliopa madarakani kwa
makusudi umekiuka katiba ya TFF kwa mara ya pili, Msajili atumie kifungu
10(1)a,b (kukiuka katiba ya Chama) za kanuni ya Usajili kuwawajibisha
viongozi hawa wa TFF waliomaliza muda wao. Kifungu
“10(1).b endapo itabainika kuwa kiongozi au viongozi wnaendesha
shughuli za chama bila kufuata katiba iliopo au kukiuka kwa makusudi
vifungu vya katiba ya chama,msajili anaweza kuchukua hatua ikiwa ni
pamoja kufutwa uongozi kwa kipindi cha uongozi
kilichobaki”.
Michael Richard Wambura.
Nakala:
:Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo
: Naibu
Waziri
:Msajili wa Vyama vya michezo na Vilabu
:BMT
No comments:
Post a Comment