MSANII wa filamu nchini, Husna Posh ‘Dotnata’ na pacha wake
Dometria Alphonce ‘DD’ sambamba na mkali wa kibao cha ‘Nitang’ara Tu’,
Mwinjilisti Kabula George, wanatarajiwa kuwasili jijini Mbeya leo tayari
kwa tamasha kubwa la kuitambulisha DVD ya ‘Nitang’ara Tu’.
Akizungumza kwa simu kutoka jijini Mbeya jana, mratibu wa tamasha
hilo, George Kayala, alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya tamasha hilo
litakalofanyika Jumapili kwenye ukumbi wa kanisa la Pentekoste
(Makimbilio), karibu ya shule ya sekondari Samora yamekamilika.
“Wasanii hao watawasili Mbeya kesho kwa ajili ya tamasha kubwa la
kuitambulisha DVD ya ‘Nitang’ara Tu’ na maandalizi kwa ajili ya shughuli
hiyo yamekamilika, hivyo nawataka wakazi wa Mbeya wajitokeze kwa wingi
siku ya Jumapili tuimbe pamoja,” alisema Kayala.
Kayala aliwataja waimbaji watakaopamba tamasha hilo kuwa ni Christina
Shusho, Ambele Chapanyota, Ipyana Mwansofu, Dotnata, Benjamin Mwakyonde
(Mzee wa Mwendo wa Farasi), Thabita Jonas, Clemence Thimotheo na Bariki
Mwakabana.
Upande wa kwaya ni Enendeni, Upendo Yeriko, Ruanda Gospel Singers na
Goshen
Kwaya, ambapo kiingilio kitakuwa sh 2,000 kwa watu wazima na
1,000 kwa watoto.
Tamasha hilo limedhaminiwa na Global Publishers, Ushindi Redio FM ya
Mbeya, DD Entertainment, Shalom Production, The Genesis Global College,
Mwasa Auto Garage, Komba Sofa Shawroom na Dotnata Entertainment.
No comments:
Post a Comment