MWANAMITINDO marufu Bongo, Jacqueline Patrick ‘Jack’ amesema
alikurupuka kuolewa na aliyekuwa mume wake, Abdulatif Fundikira ‘Tiff’
kwa kuwa hakufanya tathmini ya kina kabla ya kufanya maamuzi.

Akizungumza na paparazi wetu, Jack alisema laiti angekaa kwenye
uchumba kwa angalau muda wa miaka miwili kuchunguzana kabla ya kuoana
mwaka 2011, asingeweza kufikia hatua ya ndoa kwani wangeshindwana tabia
mapema.
“Nilikosea, nikakurupuka kuolewa mapema bila kumchunguza tabia mpenzi wangu, uhusiano wetu ulidumu miezi mitano tu kisha tukafunga ndoa, lakini matokeo yake tabia hazikuendana na ndoa ikakosa uhai ndani ya muda mfupi,”

CREDIT : Global Publishers.
No comments:
Post a Comment