SHUGHULI imeanza ndani ya Redd’s Miss Ilala 2013, baada ya
warembo 15 kutoka vitongoji vinne vya manispaa ya Ilala, kuanza maoezi
rasmi ndani ya klabu ya kimataifa ya Bilicanas jijini Dar es Salaam.
Warembo hao, wanajinoa kwa shindano hilo linalotarajiwa kufanyika ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Dar es Salaam, Agosti 16.
Kati ya warembo hao, watatu watakaoshika nafasi za juu, watapata
nafasi ya kushiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania, linalotarajiwa
kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.
Mratibu wa Redd’s Miss Ilala, Juma Mabakila, alisema warembo
wanaowania taji hilo wanatoka vitongoji vya Mzizima, Tabata, Ukonga na
Dar City Centre.
“Sisi kama kamati, tunawaomba wadau wa urembo kujitokeza kwa wingi
kuja kushuhudia muonekano mpya wa mashindano ya urembo, lakini pia
kuangalia jinsi Ilala ilivyosheheni warembo watakaoleta ushindani mkubwa
Redds Miss Tanzania 2013,” alisema.
Aliwataja warembo walioko kambi ya Redd’s Miss Ilala kuwa ni Alice
Isaac, Clara Paul, Anna Johnson, Irene Mwelolo, Munira Mabrouk, Rehema
Mpanda, Shamim Mohamed, Martha Gewe, Diana Joachim, Natasha Mohamed,
Dorice Mollel, Pendo Lema, Kazumbe Mussa na Kabula Kibogoti.
Shindano la Redd’s Miss Tanzania, kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji
cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL).
No comments:
Post a Comment