RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, ametakiwa kusikiliza ushauri wa kidiplomasia anaopewa na kuacha maneno maneno dhidi ya Rais Jakaya Kikwete. Ushauri huo ulitolewa jana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dk Richard Sezibera, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu uendeshaji wa Jumuiya hiyo.
Akizungumzia uamuzi wa Rais Kikwete kukaa kimya, licha ya maneno hayo dhidi yake, Dk Sezibera alisema yuko kimya si kwamba hataki kujibu, bali anatumia busara.
Alisema pamoja na kauli za matusi na dhihaka kwa Tanzania, Rais Kikwete hajaathiri utendaji kazi kati ya wafanyakazi wa ofisi za Makao Makuu ya EAC jijini hapa na watu wa Rwanda katika Jumuiya hiyo wanafanya kazi kama kawaida na hakuna kasoro yoyote. “Wafanyakazi wa EAC wanashirikiana pamoja na lengo letu ni kujenga Jumuiya yetu,” alisema.
Ushauri wa JK Maneno hayo kwa mujibu wa Dk Sezibera, yalianza baada ya Rais Kikwete kumshauri Kagame kukaa meza moja na vikundi vya waasi wa nchi yake (FDLR), huku akimtaka kuacha kukuza mgogoro usiokuwapo.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo kwa Rwanda takribani miezi mitatu iliyopita wakati akizungumza katika Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mapema mwaka huu, Addis Ababa, Ethiopia, ambao ulikuwa ukijadili suala la amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na ukanda wa Maziwa Makuu.
Ushauri huo pia uliwagusa Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Joseph Kabila (DRC), ambao aliwataka kufanya mazungumzo na waasi wanaopingana na serikali zao. Akizungumzia ushauri huo katika hotuba yake ya kila mwezi hivi karibuni, Rais Kikwete alisema:Akizungumzia uamuzi wa Rais Kikwete kukaa kimya, licha ya maneno hayo dhidi yake, Dk Sezibera alisema yuko kimya si kwamba hataki kujibu, bali anatumia busara.
Alisema pamoja na kauli za matusi na dhihaka kwa Tanzania, Rais Kikwete hajaathiri utendaji kazi kati ya wafanyakazi wa ofisi za Makao Makuu ya EAC jijini hapa na watu wa Rwanda katika Jumuiya hiyo wanafanya kazi kama kawaida na hakuna kasoro yoyote. “Wafanyakazi wa EAC wanashirikiana pamoja na lengo letu ni kujenga Jumuiya yetu,” alisema.
Ushauri wa JK Maneno hayo kwa mujibu wa Dk Sezibera, yalianza baada ya Rais Kikwete kumshauri Kagame kukaa meza moja na vikundi vya waasi wa nchi yake (FDLR), huku akimtaka kuacha kukuza mgogoro usiokuwapo.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo kwa Rwanda takribani miezi mitatu iliyopita wakati akizungumza katika Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mapema mwaka huu, Addis Ababa, Ethiopia, ambao ulikuwa ukijadili suala la amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na ukanda wa Maziwa Makuu.
“Ushauri ule niliutoa kwa nia njema kabisa, kwani bado naamini kuwa kama jambo linaweza kumalizwa kwa njia ya mazungumzo njia hiyo ni vema itumike.
“Isitoshe, ushauri ule niliutoa pia kwa Serikali za Congo na Uganda. Katika mkutano ule Rais Museveni wa Uganda aliunga mkono kauli yangu. Rais Kagame hakusema chochote pale mkutanoni. Baada ya kurudi nyumbani ndipo tukaanza kusikia maneno tuliyoyasikia na tunayoendelea kusikia.
“Kwa upande wangu sijasema lolote kuhusu Rwanda pamoja na maneno mengi ya matusi na kejeli yanayotoka kwenye vinywa vya viongozi wa Rwanda dhidi yangu.Si kwamba siambiwi yanayosemwa au sijui kusema au sina la kusema, la hasha, sijafanya hivyo kwa sababu sioni faida yake,” alisema Rais Kikwete.
Diplomasia si vita Akisifu ushauri huo, Dk Sezibera alisema kwanza Rwanda ilishaonja machungu ya vita na wananchi wake hawataki tena kusikia mambo ya vita, bali wanataka amani, hivyo ni vema sasa diplomasia itumike zaidi kwa Rwanda.
Alisema EAC inashauri diplomasia itumike zaidi maana ambako vita ilishawahi kutokea, hawataki tena kuona mambo hayo hivyo ni vyema Kagame afuate ushauri wa watu mbalimbali na kuachana na maneno maneno.
“Naomba haya mambo yazungumzwe kidiplomasia zaidi maana walioonja vita hawataki vita tena,” alisema na kuongeza kuwa ni vema mambo hayo yamalizwe. Wahamiaji haramu Akizungumzia hatua ya Tanzania kutaka wahamiaji haramu wote kurejea kwao na kama wakitaka kurudi nchini, wafuate utaratibu, Dk Sezibera alisema Tanzania ina haki hiyo.
Alisisitiza kuwa EAC ina wajibu wa kuangalia kwa kina kuhusu wananchi waliokimbia nchi zao na kuja Tanzania ambao hivi sasa wanarudi kwenye nchi zao. Alisema ingawa baadhi yao wanailaumu Tanzania kwa hatua iliyochukua, lakini ina haki na wajibu wa kudhibiti wananchi ambao si raia wake wanaoishi isivyo halali.
Mpaka sasa kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, wahamiaji waliorejea nchini mwao ni zaidi ya 10,672; kati yao Wanyarwanda ni zaidi ya 6,088, Warundi zaidi ya 4,000 na Waganda zaidi ya 269 ambao wametoka mkoani Kagera.
Kutoka Kigoma Warundi zaidi ya 142 na wananchi wa DRC zaidi ya wanane na kutoka mkoa wa Geita, Wanyarwanda ni zaidi ya 126 na Warundi ni zaidi ya 39.
CHANZO HABARI LEO
No comments:
Post a Comment