MWENYEKITI wa Klabu ya Soka ya Simba, Ismail Aden Rage amesema klabu hiyo haitakubali kulipwa fidia nusu nusu katika fedha zake Sh milioni 45 ambazo mshambuliaji Mrisho Ngassa anapaswa kuwalipa.
Kamati ya Sheria, Hadhi, Haki na Maadili ya Wachezaji chini ya mwanasheria Alex Mgongolwa, imemuidhinisha Ngassa kuichezea Yanga, lakini imemfungia mechi sita kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Azam FC iliyochezwa Agosti 17, mwaka huu.
Kamati hiyo ilibaini kuwa Ngassa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na Azam FC) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (Sh milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (Sh milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.
“Kamati pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo,” ilisema taarifa ya Mgongolwa wiki iliyopita.
Kutokana na hilo, jana Rage alisema kwamba Simba haitakubali tena kuchukua fedha nusu nusu kama ilivyotokea kwa suala la mlinzi Mbuyu Twite ambaye sasa anaichezea Yanga, ambaye awali alichukua fedha kwa Simba Sh milioni 30, lakini baadaye akaitosa timu hiyo na kuibukia Jangwani.
Kama ilivyo kwa Ngassa, mlinzi huyo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini mwenye uraia wa Rwanda, aliidhinishwa kuicheza Yanga na kutakiwa kurejesha fedha alizochukua kwa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, ambazo baadaye zililipwa kwa mafungu na Yanga.
“Safari hii hatutakubali kuchukua fedha nusu nusu kutoka kwa Ngassa. Tunataka tulipwe fedha zetu zote, cash (taslimu) milioni 45. Hatutaki habari kama za mwaka jana za Mbuyu Twite,” alisema Rage jana jioni akiwa njiani kwenda bungeni Dodoma, baa da ya kutua nchini akitokea Burundi ambako alikamilisha uhamisho wa nyota wawili wa Vital’O, Gilbert Kaze na Amis Tambwe ambao walikuwa hawana Hati za Uhamisho za Kimataifa (ITC) kuichezea Simba.Kamati ya Sheria, Hadhi, Haki na Maadili ya Wachezaji chini ya mwanasheria Alex Mgongolwa, imemuidhinisha Ngassa kuichezea Yanga, lakini imemfungia mechi sita kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Azam FC iliyochezwa Agosti 17, mwaka huu.
Kamati hiyo ilibaini kuwa Ngassa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na Azam FC) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (Sh milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (Sh milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.
“Kamati pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo,” ilisema taarifa ya Mgongolwa wiki iliyopita.
Kutokana na hilo, jana Rage alisema kwamba Simba haitakubali tena kuchukua fedha nusu nusu kama ilivyotokea kwa suala la mlinzi Mbuyu Twite ambaye sasa anaichezea Yanga, ambaye awali alichukua fedha kwa Simba Sh milioni 30, lakini baadaye akaitosa timu hiyo na kuibukia Jangwani.
Kama ilivyo kwa Ngassa, mlinzi huyo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini mwenye uraia wa Rwanda, aliidhinishwa kuicheza Yanga na kutakiwa kurejesha fedha alizochukua kwa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, ambazo baadaye zililipwa kwa mafungu na Yanga.
“Kamati imesema kwamba tulipwe fedha zetu zote kabla ya Ngassa kuanza kucheza, nasi tunazitaka zote. Kama Ngassa atakuwa hajalipa fedha hizo baada ya mechi sita kumalizika, tutampeleka mahakamani kwa kosa la jinai la kuchukua fedha zetu. Safari hii hatuna Msalie Mtume na mtu akiwamo Ngassa,” alisema Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini (CCM).
Kuhusu Yanga kutaka kukata rufani kuhusu uamuzi wa Kamati ya Mgongolwa, Rage alishangazwa na hatua hiyo ya mabingwa hao wa Tanzania Bara, akisema ni mbumbumbu wa kanuni.
“Nashangaa kusikia kuwa kuna watu wanataka kukata rufani. Hawajui uamuzi wa Kamati ile ni wa mwisho, labda kama wanataka kwenda CAS (Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo),” alisema Mwenyekiti huyo wa Wekundu wa Msimbazi.
Kwa uamuzi huo wa Kamati ya Mgongolwa, Ngassa ambaye pia ni mchezaji nyota wa Taifa, Stars atakosa mechi tano za Yanga katika Ligi Kuu ya Bara iliyoanza Jumamosi iliyopita ambazo ni dhidi ya Ashanti United (Dar), Coastal Union (Dar), Mbeya City, Tanzania Prisons (zote Mbeya) na Azam FC tena (Dar).
Atakuwa halali kushuka dimbani Oktoba 6, mwaka huu kuikabili Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ikiwa ni wiki mbili kamili kabla ya pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga, endapo atakuwa amekamilisha taratibu kama zilivyoelekezwa na Kamati ya Mgongolwa.
CREDIT HABARI LEO
No comments:
Post a Comment