EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, August 16, 2013

KUFURU MAZISHI YA BILIONEA

Jeneza lenye mwili wa marehemu Erasto Saimon Msuya likiwa eneo maalumu kwa ajili ya ibada ya mazishi.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
MAZISHI ya kufuru ya yule bilionea mfanyabiashara wa madini ya tanzanite mkoani hapa, marehemu Erasto Saimon Msuya, yameacha gumzo kubwa.
Mfanyabiashara huyo aliuawa kwa kumiminiwa risasi zaidi ya 20 na watu wawili wasiojulikana Agosti 7, mwaka huu maeneo ya Kia wilayani Hai, Kilimanjaro kabla ya kupumzishwa Jumanne wiki hii kijijini kwao Kairo huko Simanjiro mkoani Manyara.

Kaburi la marehemu Msuya wakati likiandaliwa.
Baada ya kutokea kwa mauaji hayo, iliundwa kamati ya mazishi ikihusisha  wafanyabiashara wa madini ya tanzanite pekee ambayo ilitengeneza bajeti ya maziko ya takribani shilingi milioni 100.
Habari kutoka ndani ya kamati hiyo zilieleza kuwa gari maalum la kifahari na jeneza lililobeba mwili vilinunuliwa Nairobi nchini Kenya.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Erasto Msuya.
KUHUSU JENEZA
Ilisemekana kuwa jeneza hilo liliagizwa na kampuni inayojishughulisha na shughuli za maziko ya Montezuma & Monalisa Funeral Home.
Ilielezwa kuwa jeneza hilo lilinunuliwa shilingi milioni nane ikidaiwa kuwa lilikuwa lina uwezo wa kufunga na kufunguliwa kwa kutumia ‘rimoti’.
Ilidaiwa kuwa jeneza hilo lilikuwa na vishikio maalum vilivyokuwa viking’aa kama dhahabu au tanzanite na kulifanya kuonekana la aina yake.


Baadhi ya waombolezaji.
MSHANGAO
Hali hiyo iliwaacha na mshangao maelfu ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wakati wa ibada iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, maeneo ya Kwaiddi, barabara inayoelekea Ngaramtoni wilayani Arumeru kabla ya kusafirishwa kwenda Simanjiro kwa maziko.

MAGARI
Pamoja na lile lililobeba mwili wa marehemu, msafara wa magari ya kifahari kuelekea kijijini huko ulisababisha Jiji la Arusha kuzizima kwa majonzi huku wengi wakishindwa kuamini kama jamaa huyo amefariki dunia na kuacha utajiri wa kutisha.
“Hebu ona, hakuna gari la ovyo, yote ni makali. Ingekuwa utajiri unaweza kumfufua mtu, basi Erasto angefufuliwa,” alisema mmoja wa waombolezaji akimwelezea jamaa huyo kuwa alikuwa mtu ‘smati’.

SUTI KUTOKA KWA MALKIA ELIZABETH
Habari za ndani zilidai kuwa hata suti aliyozikwa nayo ilitoka nje ya nchi, London, Uingereza kwa Malkia Elizabeth.
Pia ilidaiwa kuwa jamaa huyo alizikwa na cheni ya dhahabu (gold) shingoni yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10.

VYAKULA, VINYWAJI
Habari zilinyetisha kuwa huduma kama vyakula, vinywaji, mapambo na magari ya kukodishwa kutoka Arusha kwenda kijijini na kurudi viligharimu zaidi ya shilingi milioni 80.

Msema Chochote ‘MC’ Jacob Steven ‘JB’ akiwa mzigoni.
MC NI JB
Ili kuthibitisha kuwa msiba huo haukuwa wa kitoto, Msema Chochote ‘MC’ alikuwa ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’.

KAIRO, SIMANJIRO
Habari zilidai kuwa waombolezaji walipofika kijijini kwa ajili ya maziko Jumanne mchana, watu walikanyagana makaburini huku vijana wakitaka azikwe na mtu hai wa kumlinda.

KABURI
Walipofika walikuta kaburi la kifahari limeshajengwa ambapo kulikuwa na zulia maalum la kufuta miguu kabla ya kukanyaga marumaru za madini ya tanzanite zilizolizunguka.
Kuthibitisha kuwa ilikuwa ni kufuru, baadhi ya wachimbaji wadogo ‘nyoka’ walikuwa wakiwataka matajiri kulifungia kaburi hilo umeme na kiyoyozi.

MNARA WA KUMBUKUMBU
Baada ya mazishi hayo, inaelezwa kuwa familia ilikubaliana kufanya juu chini kulinunua shamba alilouliwa katika Mji wa Bomang’ombe, Mtaa wa Wasomali eneo la Mjohoroni wilayani Hai, Kilimanjaro ili kujenga mnara wa kumbukumbu.
Ilidaiwa kuwa baada ya kujenga mnara huo, familia itakuwa inatembelea eneo hilo Agosti 7, kila mwaka kwa ajili ya tambiko.

KAKA WA MAREHEMU
Kaka wa marehemu, Israel Msuya, alisema kuwa walifikia uamuzi wa kufanya mazishi hayo kwenye makaburi ya familia ya mzee Elisaria Msuya ‘Kikaango’ ambaye ni baba wa marehemu Erasto.
KUNA KULIPIZA KISASI?
Kwa mujibu wa kaka huyo wa marehemu, familia haitalipiza kisasi kwa watu waliomuua Erasto bali wao wanamwachia yote Mungu.

VIPI KUHUSU KESI?
Katika hatua nyingine, polisi mkoani hapa wanaendelea kuwahoji wafanyabiashara maarufu wa madini ya tanzanite wa mji mdogo wa Mererani wanaodaiwa kuhusika na kifo hicho.
Habari za kipolisi zilieleza kuwa mfanyabiashara mmoja wa madini, kijana ambaye aliibuka ghafla kuwa tajiri mkubwa kutokana na biashara ya madini ya tanzanite, anashikiliwa kwa mahojiano.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate