Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, Rajan Katimba (katikati) akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Wanahabari wakiwa kazini wakati wa mkutano huo.
Mjumbe kutoka Organization of Scholers in Tanzania, Ally Basalleh naye akiongea wakati wa mkutano huo.
Polisi wakidumisha ulinzi nje ya msikiti wa Mtambani ambapo mkutano umefanyika.
Viongozi wa Dini ya Kiislamu leo wamekutana
na wanahabari katika msikiti wa Mtambani Kinondoni jijini Dar, kujadili
juu ya kutolewa hospitali Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda. Sheikh Ponda alichukuliwa na
polisi kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa
(MOI) jana majira ya saa nne na nusu asubuhi. Katika taarifa yao
waliyoitoa kwa wanahabari, viongozi hao wamelaani kitendo hicho
alichofanyiwa Sheikh Ponda na kuitisha mkutano wa dharura utakaofanyika
Jumapili ya Agosti 18 mwaka huu majira ya saa 9 alasiri katika Viwanja
vya Nuruh Yakin Temeke jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA DENIS MTIMA / GPL)
No comments:
Post a Comment