MSANII wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amefunguka kuwa japokuwa
anampenda mpenzi wake wa sasa, Geofrey Kusila, hayupo tayari kubadilisha
dini yake ya Kiislamu ili aolewe.
Akichonga
na paparazi wetu hivi karibuni, Nora alisema endapo watafikia muafaka
wa kuoana na mpenzi wake huyo, hawezi kubadili dini wala kufunga ndoa ya
bomani kwa sababu anaipenda dini yake hivyo itabidi mwanaume amfuate.
“Siwezi kubadili dini na sitaki kufunga ndoa ya bomani, nataka ndoa
yetu ibarikiwe na Mungu kwa sababu nampenda Geofrey ila hatuwezi kufunga
ndoa bomani,” alisema Nora.
No comments:
Post a Comment