MWANADADA mwenye jina katika fani ya utangazaji Bongo, Maimartha
Jesse amelalamikia kitendo cha vijana wanaotumia madawa ya kulevya
‘mateja’ kulizingira duka lake lililopo Kinondoni Manyanya, jijini Dar.
Maimartha ameliambia Ijumaa juzikati kuwa, mateja hao wamekuwa
wakimuathiri sana kwenye biashara yake hiyo na kila njia aliyoitumia
kuwaondoka imeshindikana.
“Hawa mateja wananiharibia sana biashara
yangu, wateja wanashindwa kuja kununua vitu wakiwahofia, yaani
wananisabashia hasara kubwa na baadhi ya watu wanadhani na mimi nawauzia
‘unga’ ndiyo maana nawakumbatia kumbe wala,” alisema Maimartha.
No comments:
Post a Comment