UKATILI ulioje! Tajiri ambaye ni mfanyabishara mkubwa katika maduka
ya Kariakoo, Dar aliyetajwa kwa jina moja la Urio anadaiwa kumvunja
nyonga na kumjeruhi mkewe Eva Pascal anayeuguza majeraha kwenye
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akizungumza kwa uchungu akiwa wodini hospitali hapo, Eva au mama Tina
alisema kuwa tukio hilo lilitokea hivi karibuni nyumbani kwao
Kimara-Temboni, Dar.
Mama Tina alisimulia kuwa siku ya tukio mumewe alikuwa ana siku
kadhaa hajarudi nyumbani hivyo akamfuata katika Baa ya Temboni Resort
kwa ajili ya kumuuliza sababu za kushindwa kurudi nyumbani.
Alisimulia huku akitokwa machozi: “Nilipofika tu nikamuuliza swali hilo,
alinitandika kofi kisha akanipiga ngumi ya jicho hadi nikazimia.
“Nilishangaa nilipozinduka na kuwakuta manesi wamenizunguka.
Nilipomuuliza mume wangu imekuwaje aliniambia eti nililewa na kuanguka
ndiyo sababu nipo hapa.
“Kiukweli baba Tina ananinyanyasa sana, ananipiga hadi kufikia hatua ya kuniunguza na pasi. Kwa sasa naiona ndoa ni mateso makubwa na Mungu akinijalia nikapona, sitarudi tena katika mateso haya, nimechoka jamani.
“Kiukweli baba Tina ananinyanyasa sana, ananipiga hadi kufikia hatua ya kuniunguza na pasi. Kwa sasa naiona ndoa ni mateso makubwa na Mungu akinijalia nikapona, sitarudi tena katika mateso haya, nimechoka jamani.
“Ni baba Tina huyuhuyu aliwahi kuninyoa nywele na kisu eti kisa tu
nilimcheleweshea supu ambayo ilikuwa bado haijaiva ikiwa jikoni.
Alinichukua akaniingiza chumbani akaninyoa nywele na kisu kisha
akaniingiza bafuni akaniosha na maji baridi eti akidai nywele hizo
zilikuwa zinanipa kiburi.
“Yaani nikikorofishana naye kidogo tu ananitupia kila kitu nje na kufunga chumba chetu cha kulala.”
Baada ya kusikia upande wa mama Tina, Ijumaa Wikienda lilimgeukia baba
Tina ambaye alikanusha kumpiga mkewe lakini akakiri kuwa aliwahi kumpiga
na kumchoma na pasi huko nyuma ingawa walishakaa na kuyamaliza mambo
hayo.
“Safari hii sijampiga kabisa, alikuja baa akanifanyia fujo, alikuwa amelewa sana, baadaye alianguka na kuumia ndiyo nikampeleka hospitalini, hayo mengine watu wananisingizia tu,” alisema baba Tina.
“Safari hii sijampiga kabisa, alikuja baa akanifanyia fujo, alikuwa amelewa sana, baadaye alianguka na kuumia ndiyo nikampeleka hospitalini, hayo mengine watu wananisingizia tu,” alisema baba Tina.
Hata hivyo, gazeti hili halikuishia hapo kwani lilitinga eneo la
Kimara-Temboni nyumbani kwa wanandoa hao na kuzungumza na baadhi ya
majirani ambao walikiri kuwa mama Tina alipigwa na amekuwa akinyanyaswa
na mumewe kiasi cha kufikishana polisi.
Wanahabari wetu walifika polisi katika kituo kidogo cha
Kimara-Temboni ili kupata taarifa ya tukio hilo ambapo walisema kuwa
Urio alifika kituoni hapo akiwa na mkewe mahututi na kuomba PF-3 ambapo
walimpa na kumsihi mgonjwa akishapokelewa hospitalini airudishe lakini
siku iliyofuata alikwenda pale na kusema kuwa mgonjwa anaendelea vizuri.
::::GLP::::
No comments:
Post a Comment