EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, August 19, 2013

Wafuasi wa Ponda wapiga kambi Segerea

Ofisa Habari wa Magereza, Deodatus Kizinja alisema kisheria ni watu wawili tu kwa mwezi wanaoruhusiwa kumwona mahabusu mmoja.
Dar es Salaam. 
Wafuasi wa Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda wamepiga kambi katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam wakitaka kumwona bila mafanikio.


Wakizungumza jana nje ya gereza hilo, wafuasi hao walisema walipofika hapo saa nne asubuhi waliambiwa kwamba tayari ndugu zake wanne walikwisharuhusiwa kuingia kumwona.

“Tumeambiwa kwamba idadi watu hao inatosha na kwamba wengine haturuhusiwi kumwona,” alisema mmoja wa wafuasi hao, Baraka Mohamed na kuongeza: 

“Tunaendelea kusubiri huruma za askari wa Magereza labda baadaye wanaweza kuturuhusu kumwona,” alisema.

Wafuasi hao ambao walijaza sehemu kubwa ya eneo la mapokezi na nje ya gereza hilo walilalamikia kitendo cha askari hao kutokuwaruhusu kumwona kiongozi wao.

“Nimefika hapa asubuhi na mapema, lakini utaratibu sikuupenda kwa kweli. Nimezuiwa nami nataka kumwona kiongozi wangu na si mimi tu tuko wengi hapa,” alisema mfuasi huyo.


Wafuasi hao hawakukata tamaa kwani licha ya kuzuiwa waliamua kukaa jirani na lango la gereza na wengine kusimama vikundi vikundi wakijadiliana namna ya kupata nafasi ya kumwona. Sheikh Ponda ambaye alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba na Mifupa 

Muhimbili (Moi) alipelekwa katika gereza hilo Alhamisi iliyopita.
Hatua hiyo ilikuja baada ya kusomewa shtaka la uchochezi akiwa kitandani akidaiwa kutenda kosa hilo katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya Juni 2 hadi Agosti 11 mwaka huu.

Kwa nini walizuiwa?
Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Deodatus Kizinja alisema jana kuwa kisheria ni watu wawili katika kipindi cha wiki nne wanaoruhusiwa kumwona kila mahabusu.
Hata hivyo, alisema kwa kuzingatia sababu mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na wananchi, wamekuwa wakiruhusu idadi zaidi kila inapobidi.

“Kwa watu maarufu kama Ponda, Jeshi la Magereza linakuwa makini kudhibiti umati wa watu wanaotaka kumwona mahabusu kwa sababu hatuwezi kufahamu kama watu wote wana nia njema au la,” alisema Kizinja na kusisitiza kuwa ndugu zake wanne ambao walishaingia kumwona wanatosha

Msemaji wa Familia ya Ponda, Isihaka Rashid alisema alikwenda katika gereza hilo kumwona kiongozi huyo Jumamosi iliyopita lakini alizungumza naye kwa muda mfupi akaomba akapumzike...  “Jumamosi iliyopita tulimpelekea dawa, tukazungumza naye kwa muda mfupi akaomba akapumzike kwa sababu bado alikuwa anasikia maumivu,” alisema.

Lipumba ataka afutiwe mashtaka
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka Serikali imfutie kesi ya uchochezi Sheikh Ponda kwa madai kuwa ni ya kubambikiziwa.

Pia amelaani kitendo cha polisi kumwondoa Sheikh Ponda hospitali na kumpeleka gerezani huku akiwa bado anaendelea na matibabu ya jeraha alilopata.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema: “Tunaitaka Serikali ifute makosa yote ya uchochezi aliyopewa Sheikh Ponda... kwani siku zote inafahamika mtu akisema ukweli anaonekana mchochezi.”

Waumini walia na Nchimbi, Shilogile
Wafuasi wa Sheikh huyo wamepanga kuandamana nchi nzima kushinikiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile waachie ngazi.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam walisema viongozi hao wameshindwa kuchukua hatua stahili kwa polisi waliohusika kumdhuru Sheikh Ponda.

Sheikh Ponda anadaiwa kupigwa risasi na polisi mjini Morogoro Agosti 10, mwaka huu.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wafuasi wake, viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania walieleza kutokufurahishwa na jinsi Jeshi la Polisi lilivyoshughulikia suala la Sheikh Ponda.

Mwakilishi wa Jumuiya hiyo, Sheikh Kondo Juma alisema Dk Nchimbi na Shilogile wanapaswa kuachia ngazi kutokana na kumbambikia kesi Sheikh Ponda.
Sheikh Juma alisema mbali na kutaka Shilogile ajiuzulu, alitaka kamanda huyo afikishwe mahakamani kutokana na Sheikh Ponda kujeruhiwa.

“Hawa viongozi wawili wanapaswa kuwajibika. Tutaandaa maandamano nchi nzima ili kushinikiza wajiuzulu,” alisema Sheikh Juma kwenye mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englebert Kiondo.
Sheikh Juma alieleza kuwa ikiwa viongozi hao wataendelea kushikilia nafasi hizo, watakinyima kura CCM mwaka 2015.

CCM waombe radhi
Akizungumza katika mkutano huo, Kiongozi wa Kiislamu kutoka Zanzibar, Sheikh Salum Amour aliitaka Serikali ya CCM kuomba radhi kutokana na suala la Sheikh Ponda kuhusishwa na matukio ya umwagaji wa tindikali.
Pia alitishia kuwa isipoomba radhi, watainyima kura CCM kwenye uchaguzi ujao.
Credit: MWANANCHI.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate