KAMATI ya wananchi waliokombolewa maeneo yao kutoka kwa wavamizi
yaliyoko Jimbo la Kawe, imekubali Kampuni ya SKOL kuanza uhakiki wa
maeneo yao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Seif Mahungu, alisema kampuni hiyo itafanya kazi chini ya
usimamizi wa Manispaa ya Kinondoni, hivyo kuwahimiza wamiliki wote
kuhakikisha wanajitokeza wakati zoezi hilo litakapoanza.
“Kamati yetu tuliiunda kwa wananchi tuliokomboa maeneo yetu kutoka kwa
wavamizi katika maeneo ya Boko, Nakalekwa, Madale, Nakasangwe, Kinondo
na Mabwepande…tulikutana na kampuni hiyo jana na imetuhakikishia ipo
tayari kuanza kazi hiyo chini ya usimamizi wa Manispaa,” alisema.
Alisema wanatarajia kufanya mkutano mkubwa wa wamiliki wa maeneo hayo
Agosti 24, mwaka huu katika eneo la Wazo Polisi na kutaka kila mmiliki
kufika na vielelezo kamili.
No comments:
Post a Comment