Dar es Salaam.
Wakati Yanga wakigomea mechi zake kuonyeshwa ‘live’ na Televisheni ya kampuni ya Azam, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema timu itakuwa na haki na mechi zake za nyumbani pekee kama zionyeshwe au la.
Wakati Yanga wakigomea mechi zake kuonyeshwa ‘live’ na Televisheni ya kampuni ya Azam, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema timu itakuwa na haki na mechi zake za nyumbani pekee kama zionyeshwe au la.
Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema hawapingani na uamuzi wa Yanga, lakini mechi ambazo hazitarushwa ‘live’ ni zile za nyumbani pekee ambazo Yanga wana haki nazo na siyo za ugenini kama wanavyotaka.
“Sisi hatuna tatizo nao kama wameamua hivyo, lakini suala lao la kutaka mechi zote zinazowahusisha wao zisionyeshwe haitawezekana bali ni zile tu za nyumbani, lakini za ugenini siyo mali yao hivyo hawana haki nazo,”alisema Wambura.
Mwishoni mwa wiki TFF, bodi ya ligi (TPL) pamoja na Kampuni ya Azam waliingia mkataba mnono wa kiasi cha Sh168,000,000 kuonyesha mechi zote za Ligi Kuu kupitia kituo cha Azam TV, pamoja na kila klabu kuvuna zaidi ya sh 100 milioni.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema jana uamuzi uliofikiwa na kamati ya utendaji juu ya kuonyeshwa kwa mechi hizo hauna maslahi yoyote kwao. Sanga alisema kuonyeshwa kwa mechi zao kunalenga kuwakandamiza badala ya kuwanufaisha kwa maendeleo ya klabu.
TPL haikutangaza zabuni kwa televisheni nyingine za ndani na nje ili kutoa ushindani wa kweli katika kupatikana televisheni ya kuonyesha mechi hizo. “Hatukubaliani na uamuzi uliofikiwa wa kuingia mkataba bila ya kutangaziwa zabuni hizo kupitia televisheni nyingine kama ITV, TBC, Zuku pamoja na Star tv,”alisema Sanga.
Alisema kuwa mmoja wa wajumbe wa TPL ni makamu mwenyekiti wa Azam FC ambaye ahauwezi kumtenganisha na Azam Media Limited.
“Hauwezi kumtenganisha makamu mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed na Azam Media Limited, alisaini mkataba na Simba kama mkurungezi, jambo linalotufanya tusiwe na imani naye,” alisema Sanga. “Hatuoni sababu ya kuingia huko kwa sababu udhamini wao haulengi kutusaidia bali ni kutudidimiza,
sisi tunasimamia msimamo wetu wa kutoonyeshwa kwani tunaamini Yanga ni klabu kubwa,”alisema Sanga.
“Timu nyingine zote ni shindani na haingii akilini kuamini kuwa Yanga ama timu nyingine yoyote itafanyiwa usawa mbele ya Azam ambao ndiyo wamiliki wakuu,” alisema Sanga.
Kwa upande wa Mjmjumbe wa Kkamati ya Uutendaji ya Yanga, Musa Katabaro alisema Azam Media Limited haipaswi kuonyesha Ligi Kuu kwa sababu wao wana timu katika ligi hii. Katabaro alisema kwa mfano Afrika Kusini, Super Sport hairuhusiwi kuonyesha ligi ya nchi hiyo kwa sababu wana timu katika mashindano hayo.
“Bodi ya ligi kwa sasa imeteuliwa kwa muda na uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwezi Septemba, kwa nini kuwe na haraka ya kuingia mkataba na siyo tusubiri viongozi wapya watakaoingia madarakani,?” alihoji Katabaro.
No comments:
Post a Comment