Magaidi wa kundi la Al Shabaab limesema kuwa linahusika na shambulio katika jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi mchana wa Jumamosi Septemba 21, 2013 ambalo limeacha zaidi ya watu 30 kuuwawa.
Kupitia ujumbe wao katika mtandao
wa twitter, kundi hilo limesema shambulio hilo ni ujumbe kwa Serikali ya
Kenya kuitaka iondoe majeshi yake yote kutoka Somalia. Kundi hilo pia
limedai kuwa limeua watu zaidi ya idadi inayotajwa na vyombo vya usalama
vya Kenya.
Hata hivyo, Waziri wa mambo ya
Ndani wa Kenya Joseph Ole Lenku amesema serikali bado haijabaini ni nani
wamehusika na shambulio hilo.
Wakati huo huo idadi ya watu wanaosadikiwa kuuwawa imetajwa kuwa ni 30 na zaidi ya 50 wamejeruhiwa
Askari kanzu na mtutu wake mkononi akishikilia tumbo baada ya kujeruhiwa
Wateja wakihaha ndani ya duka hilo
Askari kanzu wakitafuta magaidi chumbha hadi chumba
Watu wakitembea kwa magoti na mikono mbele ya mwenzao mmoja ambaye inaonesha amedhakufa
Askari
kanzu na mtutu wake mkononi akimuokoa mtoto na mwanamke kutoka eneo la
tukio katika picha hii nadra ambayo inaeleza kila kitu. |
No comments:
Post a Comment