EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, September 27, 2013

BABA MZAZI KANIBAKA MIEZI TISA...BINTI DARASA LA TANO.


Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan KWELI dunia haina huruma! Binti wa umri wa miaka 15 tunayemtambulisha kwa jina moja tu la Zaina, mkazi wa Kimara jijini Dar ameamua kufunguka na kusimulia jinsi alivyokuwa akibakwa na baba yake mzazi aliyemtaja kwa jina moja la Mohamed, Ijumaa ndiyo lina habari hii ya kusikitisha.
 
Binti wa darasa la tano aliyebakwa na baba yake kwa miezi tisa.
ANAANZA KWA KUANIKA HISTORIA YAKE FUPI!
Akisimulia kwa uchungu, Zaina alianza kwa kuanika historia yake kwa ufupi kwamba tangu atoke tumboni, hakuwahi kumuona mama yake zaidi ya kuoneshwa kwenye picha tu!
 
Akasema hiyo yote ilitokana na hadithi aliyowahi kusimuliwa kwamba, akiwa kichanga, baba huyo alimuiba kwa mama yake anayeishi Kigamboni, Dar na kwenda kumlea Kimara kwa ushirikiano na mama yake wa kufikia.
 
Lakini akasema: Hata huyo mama wa kambo mwaka jana aliachana na baba baada ya kutufumania chumbani mimi na baba, akakasirika na kuondoka zake.
Kamanda Suleiman Kova.
SIKIA FILAMU KAMILI SASA
“Nakumbuka ilikuwa mwanzoni mwa mwaka jana, nikiwa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kimara ndipo baba alipoanza tabia ya kunilazimisha tufanye mapenzi. Alisema anataka tufanye kwa njia ya kawaida na ya kinyume na maumbile.
 
“Nilikataa lakini akawa ananilazimisha na vitisho juu. Tulianza kwa kufanya mchezo huo na baba lakini si kwa kupenda kwangu, nililazimika kwa sababu niliamini ni baba ambaye anaweza kunifanya lolote kama nitakataa, mbaya zaidi hakuwa akitumia kinga,” alisema na kuongeza:
 
“Kuanzia hapo, zoezi hilo liliendelea kila siku hadi mwishoni mwa mwaka jana nilipoamua kutoroka na kwenda kuwaeleza ndugu wa baba, kule Tanga.”
Binti huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa,  kilichomsukuma kutoroka ni mateso, ukatili na udhalilishwaji uliopitiliza kwani baba yake wakati akimwingilia alikuwa akimkaba kooni ili asipige kelele.

“Yeye alijua anafanya kosa, akawa akiniingilia huku ananikaba koo nisipige kelele. Nilikuwa nasikia maumivu makali balaa,” alisema binti huyo.
ALIWAAMBIA MAJIRANI LAKINI WALIOGOPA KUMVAA BABAKE
“Kingine kilichonifanya nitorokee Tanga kuwaambia ndugu zake ni kwamba, niliwahi kuwaambia majirani kuhusu mchezo wa baba lakini hakuna aliyethubutu kumuuliza kwa vile wanamuogopa,” alisema.

MAMA MZAA BABA AAMBIWA KILA KITU
Zaina alizidi kusema kuwa, baada ya kufika Tanga  alimweleza kila kitu bibi yake (mama mzaa baba’ke). Bibi huyo kwa sababu ni mzazi alimwita mwanaye na kumkanya kisha akafanyiwa mambo ya kimila ili kuondoa balaa hilo la baba mtu kutembea na mwanaye wa kumzaa la sivyo kwa mila za kwao ukoo mzima ungesambaratika.

BABA MTU AONDOKA TANGA USO UMEMSHUKA, YEYE AGOMA
“Baada kufanyiwa mambo ya mila, baba aliniambia turudi Dar lakini nilikataa kwa sababu niliamini tutakapofika bado atataka kuniingilia tena. Nasema hivyo kwa sababu pia baba amewahi kufanya mapenzi na dada’angu anaitwa Hamida mpaka akampa mimba.
 
“Huo ukatili wote alikuwa akitufanyia kwa nyakati tofauti tofauti, dada alipopata mimba siku moja alimwibia fedha ili akaitoe, alifanikiwa na akakimbia nyumbani, sijui alipo,” alisema.
 
Akaendelea: Basi, niliamua kubaki kwa bibi, lakini kuna siku alikuja mtu aliyekuwa anatafuta msichana wa kazi ‘hausigeli’, mimi nikakubali, nikaenda Moshi ambako nilikaa kwa muda.

“Hivi karibuni nilirudi Dar na kufikia kwa jirani, sikutaka kwenda nyumbani kwa baba, namuogopa atataka tena. Huyu jirani niliyefikia kwake, mtoto wake ni rafiki yangu tulikuwa tunasoma naye. Hapa nilipo natafuta msaada wa kumpata mama yangu mzazi. Kama atabahatika kulisoma gazeti hili namuomba anifuate jirani na kwa baba atanipata,” alisema Zainab.
 
Zainab hakuishia kwenye kufikia kwa jirani tu, anasema akiwa hapo jirani huyo kesho yake alimpeleka serikali za mitaa ili kutoa taarifa kuwa amerudi kwa vile alitafutwa kwa muda mrefu kwenye shule aliyokuwa akisoma.
MWENYEKITI WA MTAA AKIRI ZAINAB KUBAKWA NA BABA’KE
Naye mwenyekiti wa mtaa wa eneo hilo, Demetrius alikiri kumpokea mtoto huyo na kumsimulia yote kuhusu baba yake ambapo aliambatana naye hadi Kituo cha Polisi Mbezi kwa Yusuf kwa lengo la kutoa taarifa ili mzee huyo achukuliwe hatua za kisheria. Alisema binti huyo alifunguliwa jalada la kesi KMR/RB/114/2013  UCHUNGUZI.

BABA ANASEMAJE?
Baada ya kumalizana na binti huyo aliyeungwa mkono na mwenyekiti huyo, mapaparazi wetu walizungumza na baba mtuhumiwa ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Si kweli, huyo mtoto ananisingizia tu, mimi siwezi kufanya kitu kama hicho na binti yangu wa kumzaa hata siku moja.

KUHUSU MIMBA NA BINTIYE HAMIDA?
“Kuhusu mimbaaa…, pia si kweli. Ile mimba ilikuwa ya  kijana mmoja wa mtaani ambapo baada ya kugundua nilimfukuza nyumbani kwangu.”
CHANZO NI GLP

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate