Mastaa wa kada mbalimbali Bongo, akiwemo mtangazaji Maimartha Jesse,
mwigizaji Nuru Nassoro ‘Nora’, wanamuziki Elias Barnaba, Aneth Kushaba
wa Skylight Band na wanawake wa mjini, Maila Msafiri na Devotha,
wanadaiwa kuaibika kisa madeni.
Habari zinadai kuwa mastaa hao wamekuwa wakihenyeshwa na madeni ya
nguo kutoka kwenye duka moja lililopo maeneo ya Kinondoni, Dar
linalomilikiwa na mtangazaji ambaye pia ni mwigizaji, Lulu Mathias
Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Akizungumza na gazeti hili huku akidondosha chozi, Aunty Lulu alisema anasikitishwa na kitendo hicho alichofanyiwa na mastaa wenzake.
“Niliwaamini, nikawakopesha nguo lakini wamekuwa wakinisumbua kwenye kunilipa. Inauma sana kwa sababu wanataka kunirudisha nilikotoka.

Mwigizaji Nuru Nassoro ‘Nora’.
“Nimewavumilia sana, hii ni biashara, wanadhani nitafanyaje mimi?” alihoji Aunty Lulu.
Aunty Lulu aliomba wamlipe kwani fedha hizo ndizo amekuwa akitumia kununulia mzigo mwingine ili asifilisike.
Baada ya kuwataja wadeni wake, Jumatano wiki hii gazetini hili lilifanya jitihada za kuzungumza na mmoja baada ya mwingine ambapo walikuwa na haya ya kusema:
Nora: “Jamani Aunty Lulu nitamlipa kesho (Alhamisi) asubuhi, kwa nini anataka kutoa gazetini? Hizi siku nne tu anaona ni nyingi? Niko location (eneo la kurekodia filamu) nilimwambia anivumilie nitamtumia kwa simu sijapata muda tu.”
Barnaba: “Sidhani, nilitegemea utaniuliza unatoa lini wimbo mpya, kwa hilo sina comment (maoni).”
Anneth: “Kila mtu ana madeni duniani, kesho (Alhamisi) njoo saa nne Mlimani City (Dar), uje umchukulie fedha zake.”
Jamilah: “(Anacheka) Hahahahaa… Aunty Lulu bwana, atakuwa anatania, mimi hanidai.”
Maimartha: “Mimi huwa nampa Aunty Lulu fedha nyingi sana zaidi ya hizi anazonidai, nampenda sana siwezi kumuangusha katika biashara yake.”
Kwa upande wake, Devotha ambaye ni dada wa mjini alipotafutwa kwa njia ya simu ya kiganjani hakupatikana.

CHANZO NI GLP
No comments:
Post a Comment