WAKATI mwanasoka Joseph Kaniki ‘Golota’, bondia Karim Matumla na
msanii Agnes Gerald wakifikishwa mahakamani juzi (Jumatano) katika nchi
mbili tofauti barani Afrika, wana Bongo Fleva maarufu nchini, Chegge
Chigunda na Hassan Bilal ‘Shetta’, Jumanne iliyopita walikiona cha moto
baada ya kuhisiwa kubeba ‘poda’ na hivyo kufanyiwa upekuzi mkali katika
Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Habari
zilizopatikana juzikati zinasema, Chegge na Shetta walisafiri salama
kwa boti kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar wakiwa safarini kuelekea
Mombasa walikoalikwa kwa ajili ya shoo.
“Wale askari wa uwanjani baada ya kuwaona wasanii hao waliwatilia shaka kwa nini wapandie ndege Zanzibar badala ya Dar es Salaam, wakahisi wamebeba mzigo, basi walifanyiwa upekuzi mkali, mizigo yao ilitolewa kila kitu, kwa kweli walihenya ile mbaya.

“Lakini kitu cha kushangaza ni kwamba waliopekuliwa namna hiyo ni wao
tu, watu wengine walisachiwa kidogo na kuachiwa wapite. Pamoja na
kwamba ni vita nzuri ya kupambana na mihadarati lakini wakati mwingine
ni ‘too much’,” kilisema chanzo chetu kilichoshuhudia tukio hilo.
Chegge.
Hata hivyo, baadhi ya mashuhuda walisema Chegge na Shetta walisafiri
kwa boti hadi Zanzibar na baadaye kupanda ndege kuelekea Mombasa kwa
vile ipo ndege inayokwenda na kurudi baina ya miji hiyo miwili tu ya
pembezoni mwa Bahari ya Hindi.
CHANZO NI GLP
No comments:
Post a Comment