
 Kwa mara ya kwanza katika historia 
ya Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa za afya ya Jamii (IANPHI),
 Tanzania imepewa heshima ya kuratibu mkutano wa nane wa mwaka wa  
taasisi hiyo  na kupata nafasi ya kuing'arisha nchi katika ramani ya 
dunia na hatimaye kuweza kutangaza maliasili zake na vivutio vya Utalii 
vilivyomo. Mkutano huo wa nane wa IANPHI unataraji kufanyika kuanzia 29 
Septemba 2013 hadi 1 Oktoba mwaka huu jijini Arusha katika Hoteli ya 
Ngurdoto. 
 Akizungumza hii leo jijinni Dar es Salaam,
 Makamu wa Rais, Chama cha Kimataifa cha Taasisi
za kitaifa za Afya ya Jamii(IANPHI) na Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa
 ya
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dr. Mwele Malecelaamesema 
mkutano huo utashirikisha washiriki 150 kutoka nchi 73 wanachama. 
 Daktari. Mwelecele Malecela ameimabia Father Kidevu Blog,
 katika ofisi zake za NIMR jijini Dar es Salaam hii leo kuwa mkutano huo
 unataraji kufunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Daktari. 
Hussein Mwinyi.
Makamu huyo wa Rais wa IANPHI 
Daktari. Mwele amesema kuwa wanachama wa taasisi hiyo watakao shiriki 
katika mkutano huo hususan wakuu wa Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii 
watapa fursa ya kujadili masuala muhimu ya afya ya jamii: kugbadilishana
 uzoefu na kubuni mbinu za kitaalam za kukabiliana na changamoto 
zilizopo katika sekta ya afya ya jamii.
"Mkutano pia utatoa nafasi kwa 
washiriki kujadili mbinu za kukuza ushirikiano ili kuimarisha afya ya 
jamii kuelekea mwaka 2015, ambapo mataifa yamejiwekea nia ya kukamilisha
 utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia (MDG's).
Kauli mbiu katika mkutano huo wa mwaka 2013 ni "Afya ya Jamii baada ya mwaka 2015 na mabadiliko ya majukumu ya Taasisi za kitaifa za afya ya Jamii" 
Chama hicho cha IANPHI kina wanachama 81 huku makao makuu ya Sekretarieti yake yakiwa mji wa Helsinki, Finland.
 
 
 
 
 
 
 



 
No comments:
Post a Comment