HOST wa kipindi cha Wanawake Live cha East Africa Television,
Joyce Kiria amejikuta akichezea matope miguuni alipokuwa anarekodi moja
ya vipindi vyake.
Tukio hilo ambalo alilifanya bila kukusudia, lilitokea hivi karibuni
katika Kijiji cha Machali B, mkoani Dodoma wakati alipokwenda kuchunguza
tatizo la kukauka kwa maji katika bwawa lililopo kijijini hapo.
“Unajua kile kijiji wakazi wake wanalalamika sana kuhusiana na maji
ambayo wanakunywa kwa vile bwawa hilo limekauka kabisa na kuna wakati
wanachota matope matupu, inasikitisha,” alisema Kiria.
“Nilipojaribu kukanyaga nilijua ni sehemu kavu kumbe ni matope ya nguvu, nilikumbana nayo kwenye miguu yangu yote,” alisema.
No comments:
Post a Comment