Stori: Imelda Mtema
MasIkini! Baba mzazi wa Miss Tanzania mwaka 2006 ambaye pia ni staa mkubwa wa filamu, Wema Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu yupo kitandani akiwa amepooza upande mmoja wa mwili wake.
MasIkini! Baba mzazi wa Miss Tanzania mwaka 2006 ambaye pia ni staa mkubwa wa filamu, Wema Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu yupo kitandani akiwa amepooza upande mmoja wa mwili wake.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, mwishoni mwa wiki
iliyopita aliiwakilisha serikali kwenda kumjulia hali mzee huyo ambaye
aliwahi kuwa Waziri wa
Habari, Utamaduni na Michezo visiwani Zanzibar na
balozi katika nchi mbalimbali ambaye yupo nyumbani kwake Sinza-Mori,
Dar.
Katika hali ya kusikitisha, mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu,
aliliambia gazeti hili ambalo lilikuwa limeongozana na Nchimbi kuwa,
mume wake alipatwa na ugonjwa huo akiwa kazini Zanzibar, ingawa kwa muda
mrefu amekuwa akisumbuliwa na kisukari.
Alisema baada ya kupata
taarifa za ugonjwa huo, familia ilipanda ndege kutoka Dar kuelekea
Zanzibar ambako walimchukua na kumpeleka Hospitali ya TMJ ya jijini Dar,
alikolazwa kwa muda wa wiki tatu kabla ya kuruhusiwa.
“Ingawa bado
amepooza, lakini kwa sasa hali yake ni afadhali kuliko alivyokuwa mara
ya kwanza,” alisema mama huyo aliyedai kuwa mumewe ni mgonjwa kwa mwezi
mmoja sasa na kwa kipindi chote hicho, amekuwa akifanyiwa kila kitu.
WASIFU MFUPI WA MZEE SEPETU
Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo
miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu
Julius Kambarag Nyerere. Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi
tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere.
Pia, Machi 27,
mwaka huu, Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dr Mohammed
Shein, kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya
Uwekezaji Vitegauchumi ya Zanzibar (ZIPA).
No comments:
Post a Comment