Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kukabiliana na magaidi walioteka nyara baadhi ya wakenya katika jengo la Westgate
Katika ukurasa huu tutakupasha moja kwa moja matukio yanavyojiri katika jengo la Westgate.
15:33 Waziri wa usalama wa Kenya Joseph Ole Lenku asema kuwa wanajeshi wameweza kudhibiti jengo lote la Westgate
15:20 Polisi waonekana wakikimbia huku na kule katika harakati zao hizo dhidi ya Al Shabaab
14:56 Mkuu wa majeshi Meja Jenerali Julius
Karangi amesema magaidi hao wanaweza kujisalimisha ikiwa wanataka kwa
sababu jeshi litakabiliana nao vilivyo. Pia amesema kuwa Kenya
inakabiliana na magaidi wa kimataifa
14:35 Ole Lenku anasema kuwa hali ingali tete
lakini vikosi vya usalama vya Kenya vinakaribia kuwazingira magaidi
hao...Hadi kufika sasa watu 62 wamefariki na wengine zaidi ya 175
kujeruhiwa. Pia ameongeza kuwa magaiodi wote ni wanaume, kutokana na
taarifa za awali kuwa magaidi hao walikuwa wanaongozwa na mwanamke
14:30 Ole Lenku anasema kuwa wanajeshi kumi
wamejeruhiwa na wanapokea matibabu. Pia mateka karibu wote wameweza
kuokolewa. Ole Lenku pia amesema kuwa wameweza kuwaua magaidi wawili
14:28 Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku anasema
kuwa moshi ulitokana na moto uliosababishwa na magaidi wlaioko ndani ya
jengo hilo kujaribu kusambaratisha juhudi za wanajeshi wa Kenya dhidi
yao
14:03 Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa
vikosi vya usalama vinakaribia kudhibiti jengo hilo lote na vimeingia
ndani kabisa ya jengo hilo kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka
14:00 PM: Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo
13:54: Mwandishi wa BBCIdriss Situmaaliye katika
eneo la Westgate anasema duru zinaarifu kuwa vikosi vya usalama vya
Kenya vinasema kuwa ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia
ndani kabisa ya jengo hilo
13:52 PM Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda
katika eneo la shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya
usalama vinawataka watu kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili
kuwawezesha kufanya kazi yao
13:49 pm: Moshi mkubwa mweusi waonekana ukitoka juu ka juu katika jengo hilo haijulikani nini kilichosababisha
13:19 pm Moshi mkubwa unaonekana ukitoka katika
jengo la Westgate ambako wapiganaji wa Al Shabaab wanawazuilia mateka
wakenya ambao idadi yao haijulikani
13:12 PM Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al Shabaab
12:30 PM: Milipuko zaidi na milio ya risasi
imesikika katika jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya
jitahada za misho kuwa.
CHANZO CHA HABARI NI BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment