EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, September 30, 2013

RAIS KIKWETE: ICC INAHARIBU MAHUSIANO YAKE NA AFRIKA.


 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mwenendo wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kuhusu Bara la Afrika na viongozi wake, unainyima Mahakama hiyo nafasi kubwa ya kuungwa mkono na Bara la Afrika.

Rais Kikwete pia amelaani vikali mashambulizi yanayoongezeka dhidi ya vikosi vya kimataifa vya kulinda amani katika nchi mbali mbali duniani wakiwamo walinda amani wa Tanzania.

Rais Kikwete alitoa msimamo huo wa Tanzania mwishoni mwa wiki wakati alipohutubia Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) mwaka huu, kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.

Katika hotuba yake fupi na iliyowavutia wasikilizaji, Rais Kikwete alisema kuwa ni dhahiri kuanzishwa kwa ICC kutokana na Mkataba wa Rome kulikuwa ni hatua muhimu sana katika mfumo wa kimataifa wa kupambana na makosa ya jinai.

“Kwa hakika kuundwa kwa Mahakama hiyo kuliweka mfumo mzuri wa kuondokana na watu kutenda vitendo vya jinai na kuweza kuepukana na kuwajibika kwa vitendo hivyo na Mahakama hiyo ilianzishwa kwa kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na Afrika.

“Hata hivyo, muongo mmoja tu baada ya kuanzishwa kwa Mahakama hiyo, ni dhahiri kuwa mvutano umezuka kati ya ICC na Bara la Afrika. Sasa Mahakama hiyo inaonekana kama taasisi isiyojali maoni na msimamo wa Afrika, kwa mambo ambayo kwa maoni yangu, ni hofu halali ya Waafrika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Bado Mahakama hiyo inaendelea kupuuza maombi ya mara kwa mara ya Umoja wa Afrika. Ni jambo la kutia huzuni kuwa maombi ya kubadilisha muda wa kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Naibu Rais William Ruto yalipuuzwa na hata hayakujibiwa kabisa.”

Ameongeza Rais: “Tabia hii imekuwa ni hitilafu kubwa ambayo inaleta kikwazo kwa ICC kushindwa kutimiza wajibu wake wa kupambana na tabia ya watu wanaofanya makosa ya jinai kutokuchukuliwa hatua. Kwa hakika, kugangamara kwa ICC hata katika masuala yaliyo wazi, kumethibitika kuwa kunainyima Mahakama hiyo nafasi ya kuendelea kuungwa mkono Barani Afrika.”
    
Rais Kikwete alisema pia kuwa Tanzania sasa imekuwa moja ya nchi ambazo zinashiriki zaidi katika shughuli za kimataifa za kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa. Tanzania ina zaidi ya walinda amani 2,500 katika Darfur, Sudan; Lebanon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na kuwa ni nchi ya sita katika Afrika na ya 12 duniani kwa kutoa walinzi wa amani duniani.
   
 “Kwa hakika tunaridhishwa na mchango wetu mdogo katika shughuli hii. Na tunajua kuwa wakati mwingine tunalipa gharama kubwa na maisha ya vijana wetu kwenye shughuli hizi kama ilivyotokea majuzi katika Darfur na DRC. Waliopoteza maisha yao ni mashujaa wa taifa letu ambao maisha yao hayakupotea bure.”
   
 Aliongeza Rais Kikwete: “Vifo vya walinda amani wetu ni ukumbusho wa kutosha wa hatari zinazowakabili walinda amani wote duniani. Ni jambo la kuudhi, kwamba vikundi vyenye silaha na waharibifu wa amani duniani wanaongeza mashambulizi hayo dhidi ya watumishi wa amani. Ni lazima tulaani mashambulizi haya kwa nguvu zetu zote kwa sababu hakuna  sababu yoyote ya kuhalalisha mashambulizi haya ya kinyama ambayo ni kosa la kimataifa la jinai chini ya Sheria za Kimataifa.”
  
  Alisisitiza: “Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo wajibu wake mkuu ni kulinda amani na usalama wa kimataifa lazima liwe mstari wa mbele katika kulaani vitendo hivyo vya kinyama na haraka tu vinapotokea.”
    
Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi katika Marekani na Canada ameondoka New York usiku wa leo, Jumamosi, Septemba 28, 2013, kurejea nyumbani ambako atawasili Jumatatu mchana.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Septemba, 2013

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate