Na Mashaka Mhando,Korogwe
DADA wa Mwenyekiti wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amefariki papo hapo
baada ya gari alilokuwa akiendesha kupasuka tairi ya mbele na kuingia
chini ya daraja baada ya kupinduka na kusababisha watu wawili kufa na
wengine watatu kujeruhiwa vibaya.
Dada
huyo, Grace Aikaeli Mbowe, anayesadikiwa kuwa na umri kati ya miaka 47
hadi 50, alikuwa akiendesha gari yenye namba T 277 CAJ aina ya Toyota
Cresta akiwa na mumewe aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Lukindo (52),
wakitokea Jijini Tanga, walipata ajali hiyo eneo la Kabuku wilayani
Handeni.
Kamanda
wa polisi mkoani Tanga (ACP) Costatine Massawe alisema kupitia Ofisa
wake wa upelelezi mkoani Tanga, Bw Aziz Kimata, kwamba
ajali hiyo ilitokea majira ya saa
1:30 leo asubuhi katika eneo hilo baada ya gari hilo kupasuka tairi ya
mbele kulia na kisha kuingia chini ya daraja lililokuwepo eneo hilo.
"Ni kweli
kuna ajali ilitokea eneo la Kabuku gari aina ya Cresta lililokuwa
likiendeshwa na ndugu inavyosemekana wa Bw Freeman Mbowe, limepata ajali
baada ya kupasuka tairi la mbele na kuacha barabara na kuingia chini ya
daraja dereva anayeitwa Grace Aikael Mbowe na mtu anayesemekana ni
mumewe anayeitwa Ibrahim Lukindo, wamefariki na watu watatu
waliowachukua wamejeruhiwa," alisema RCO Kimata.
Aliwataja
waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Bw Ridhiwani Bakari (29) aliyekuwa na
mkewe Zeddy Nzuke (29) raia wa Kenya aliyekuwa na mtoto wake mwenye umri
wa miaka miwili na miezi minne aliyefahamika kwa jina la Mariam
Ridhiwan ambao kwa sasa wamelazwa katika hospitali ya Magunga wilayani
Korogwe.
RCO
Kimata aliyezungumza kwa niaba ya kamanda huyo wa polisi alisema chanzo
cha ajali hiyo inasemekana kimetokana na kupasuka kwa mpira huo na
mwendo kasi wa kawaida na kwamba majeruhi na maiti zi9mehifadhiwa kwenye
hospitali hiyo.
Mwandishi
wa habari hizi, aliyefika kwenye hospitali hiyo na kuzungumza na
Ridhiwani pamja na mkewe ambaye amelazwa wodi namba mbili ya wanawake
katika hospitali hiyo, alisema kwamba ndoto zake za kufanya kazi Dar es
salaam zimezimika ghafla kutokana na kwamba alikuwa aende kupamba kazi
ya uofisa ugavi katika taasisi moja ya fedha ya marehemu Mbowe Jijini
Dar es salaam.
"Nilikuwa naenda kupewa kazi na mama Mbowe katika Institution yake ya
Micro-Financial Jijini Dar es salaam, mimi ni procurement
(Mgavi-manunuzi) na ni Mkenya kwetu ni Eastern Province Kang'undo na
nimeolewa na bwana Mtizedi...Lakini sasa ndoto zangu za kufanya kazi Dar
es salaam zimezimika ghafla," alisema Zeddy akiwa kitandani amelala na
mwanwe ambaye alikuwa haongei tangu amefika katika hospitalini hapo.
Mumewe na mwanamke huyo akizungumzia ajali hiyo alisema kuwa hakuwa
akijua kwani alikuwa amelala dakika tatu kabla ya kutokea ajali hiyo
ambapo alishtukia yeye, mkewe na mwanawe wametupwa chini kwenye majani
wakiwa hawajijui na walikimbizwa katika hospitali hiyo ya Korogwe.
Ridhin ambaye ni mkazi wa Nguvumali Jijini Tanga, alisema safari yao
hiyo ilikuwa ifanyike Jumamosi mchana lakini kutokana na na kuchelewa
kwa wenyeji wao hao, waliondoka Tanga kwenye hoteli ya Doliphin
walikolala majira ya saa 11:00 alifajiri kwa ajili ya kwenda Jijini Dar
es salaam.
Muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo Bi Nayela Missingo alikiri kuwapokea
wagonjwa hao ambapo alisema wanafanya jitihada za kuwahamishia katika
hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam mtoto Mariam ambaye
amepata majeraha katika kichwa chake na kwamba tangu afikishe hospilaini
hapo hakuwa katika hali nzuri, haongei walakunyonya.
Bi Zeddy Nzuke na mtoto wake wakiwa wamelazwa katika hospitali ya
Magunga wilayani Korogwe baada ya kupata majeraha katika ajali hiyo.
Muuguzi wa zamu katika hospiotali ya magunga wilayani Korogwe Nayela Missingo akimsaidia kukaa kwenye kitanda Bw Ridhiwani Bakari baada kuopata ajali hiyo |
No comments:
Post a Comment