IMG_9492
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar. Kushoto ni Mtaalamu wa Ofa kutoka Tigo, Bi. Jacqueline Nnunduma.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, alisema kwamba waliona umuhimu wakuanzisha kodi hii mpya ili kuwarahisishia wateja wake kuweza kupata bidhaa na huduma mbali mbali kutoka Tigo kupitia menyu moja tofauti na kutumia nambari tofauti tofauti kama ilivyozoeleka hapo awali.

“Kama mnavyofahamu, kampuni ya simu ya Tigo ina huduma mbali mbali, kwahiyo kitu tulichokifanya ni kumrahisishia mteja kutokupoteza muda na kuondokana na usumbufu wa kukariri nambari tofauti tofauti za huduma zetu kwa kuyakusanya huduma zote na kuziweka katika menyu moja,” alisema Mpinga.

“Kitendo cha kupiga *148*00# wateja wetu watakuwa na uwezo wakupata huduma na bidhaa za Tigo kwenda Tigo, pamoja na za Tigo kwenda mitandao mengine kama vifurushi vyetu vya Xtreme na Mini Kabaang. Huduma zingine ambazo zitapatikana katika hii kodi mpya ni vifurushi vya Intaneti, Burudani na Nunua pitia Tigo Pesa,” aliongeza.

Kutokana na maelezo ya Mtaalamu wa Ofa kutoka Tigo, Bi. Jacqueline Nnunduma, huduma hii mpya ni sawa na kwenda katika duka moja na kupata kila bidhaa unayoihitaji bila kupoteza muda wakuzunguka maana kila kitu kinapatikana papo kwa papo. 

“Kodi hii ya *148*00# pia imetengenezwa mahususi kwa ajili ya kumpatia mteja aina tofauti tofauti ya huduma na bidhaa kutokana na salio lake na eneo anayopatikana kwa wakati  huo,” alisema.

“Kwa mfano, kwa wateja wetu wa Kanda ya Ziwa na Arusha, huduma kama ya Tatu Kali itaonekana moja kwa moja katika menyu zao; huku wateja ambao hawatakuwa na salio la kutosha watapatiwa chaguo la huduma ya Niwezeshe,….na mengine mengi,” alisema Nnunduma.

Nnunduma pia aliendelea kusisitiza kwamba bidhaa za Tigo zitaendelea kutolewa kwa mfumo wa vifurushi vya Siku, Wiki na Mwezi ili kuweza kutimiza mahitaji ya kila aina ya mteja kutoka Tigo.

“Pamoja na kwamba kila huduma na bidhaa zitawekwa katika menyu moja, suala la kwamba bado tutakuwa tunatoa huduma hizi pitia vifurushi vya Siku, Wiki na Mwezi ni jambo ambalo haliwahakikishii tu upatikanaji kwa urahisi wa huduma zetu kwa wateja wet bali pia ni uhakika wa kufikisha huduma zetu kwa kila mmoja kwa bei nafuu,” alimalizia Nnunduma.

CREDIT Mo Blog.