Mkurugenzi
wa masoko wa Airtel, Levi Nyakundi akiongea wakati wa hafla ya
kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising Stars mara baada ya
kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria,
hafla hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt.
Katibu
Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini, Angetile Osiah akiongea
wakati wa hafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising Stars.
Kocha
wa timu ya wasichana ya Airtel Rising Stars, Rogatician Kaijage
akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel
Rising Stars.
Wachezaji
waliozawadia kwa kungar'a katika michuano ya Airtel Rising Stars pamoja
na nahodha wa timu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini, Leonard Thadeo (mwisho
kushoto) katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile
Osiah.
Naodha
wa timu ya wasicha ya Airtel Rising Stars chini ya umri wa miaka 17
Stumai Abdallah akimkabidhi kombe la ubingwa Mkurugenzi wa maendeleo ya
michezo nchini Leonard Thadeo baada yakuwa mabingwa katika mashindano
yaliofanyika nchini Nigeria Jumapili. Kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa
Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira
wa miguu nchini Angetile Osiah.
Kaptain
ya timu ya wasichana Stumi, akikabithi cheti cha kushinda kwa
Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo baada ya kuwa
mabingwa katika mashindano yaliofanyika nchini Nigeria Jumapili. Kushoto
ni mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu
mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Mchezaji
wa timu ya wasichana Neema Paul pamoja na Mkurugenzi wa maendeleo ya
michezo nchini Leonard Thadeo wakionyesha mfano wa hundi ya dola 10,000
iliyokabidhiwa kwa timu ya washichana na Airtel baada ya kuibuka
washindi wa michuano ya Airtel Rising Stars Afrika. Kushoto ni
mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu
wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Wachezaji
wa timu ya wavulana wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla
ya kuwapongeza iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam,
pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini
Leonard Thadeo, wakurugenzi wa Airtel, mkuu wa shirikisho la mpira wa
miguu nchini Angetile Osiah pamaoja na Salim Madadi wa TFF
- Serikali yaipongeza timu ya wasichana ARS
- Yashauri sekta binafsi kusaidi katika michezo.
Mkurugenzi wa maendeleo wa michezo nchini bw Leonard Thadeo
ameipongeza timu ya wasichana ya Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa
vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars yaliomalizika
juzi nchini Nigeria.
Tanzania waliibuka mabingwa baada ya kuwafunga Kenya katika fainali,
pia amewapongeza wavulana baada ya kufikia hatua ya nusu fainali.
Mabingwa wamezawadiwa kombe pamoja na kitita cha dola za marekani
10,000.
Katika pongezi zake pia amewapongeza wafungaji kwa upande wa wasichna
ni Shelda Boniface na mvulana ni Athanas Mdamu na pia amempongeza
mchezaji bora kutoka timu ya wasichana ambae ni Tatu Iddi .
Katika mashindano haya Tanzania imetoa rekodi tatu , mfungaji bora
kwa upande wa wasichana magoli matano, mfungaji bora wa kiume magoli
manne , mchezaji bora kwa upande wa wasichana na pia wachezaji watatu
upande wa wavulana wamefunga magoli matatu katika mechi moja (hat-trik)
na kuondoka na mpira kila mmoja.
Kabla ya kukabidhiwa kombe na mabingwa hao , Mkurugenzi wa maendeleo
ya michezo nchini bw Leonard Thadeo amesema kuwa serikali kupitia wizara
ya michezo itaendelea kusaidi mpira wa vijana wenye umri mdogo ili
kuifikisha mbali Tanzania katika medani ya soka.
Akiongea kwa niaba ya msafara wa timu kocha Rogacian Kaijage amesema
kua mashindano yalikua magumu ila wamefanikiwa kuchukua ubingwa ,
amewapongeza vijana wake , kocha mwenzie wa timu ya wavulana Abel Mtweve
na pia ameishukuru Serikali , Airtel , TFF, pamoja na DRFA.
Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Bw. Levi Nyakundi ameahidi kuwa Airtel
itaendelea kudhamini mpira hasa wenye umri mdogo na pia kuongeza mikoa
ya ushiriki wa mashindano ya Airtel Rising Stars
No comments:
Post a Comment