EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, September 24, 2013

Simu za watu milioni 8 kufungiwa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu

WATUMIAJI wa simu wapatao milioni nane wapo hatarini kufungiwa simu zao ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Tayari Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeziandikia kampuni za simu waraka wa kuzitaka zianze kukata kodi mpya ya laini (simu card) mara moja kuanzia Julai 30, 2013.

Hatua hiyo inatokana na serikali kushindwa kufuta kodi hiyo ya sh 1,000 iliyopitishwa na Bunge kama alivyoagiza Rais Jakaya Kikwete baada ya kukutana na wadau wa sekta ya mawasiliano.

Kwa maana hiyo kila anayemiliki laini moja ya simu atakatwa sh 3,000; anayemiliki laini mbili sh 6,000 na anayemiliki laini tatu sh 12,000, lengo ni kuhakikisha serikali inakusanya sh bilioni 178 zitakazopelekwa kwenye bajeti kuu ya serikali.

Watumiaji wa simu sasa watalazimika kulipia kodi hiyo ya miezi mitatu ya Julai, Agosti na Septemba kwa wakati mmoja.

Bunge kupitia Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) lilitaka kuwapo kwa kodi hiyo ili kusaidia shughuli za bajeti ya Serikali Kuu.

Kupitishwa kwa kodi hiyo kuliibua malalamiko ya wanasiasa dhidi ya Chenge anayelazimisha kuwapo kwa kodi hiyo, huku akishindwa kuamini kwamba kuna Mtanzania anayekosa sh 1,000 kwa mwezi kwa ajili ya laini ya simu.

Malalamiko hayo yaliendelea hadi kwa wananchi na baadhi ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliotaka posho za wabunge zipunguzwe ili kuziba pengo hilo badala ya kuwabebesha wananchi mzigo.

Inadaiwa kwamba msimamo wa Chenge unaungwa mkono na Spika wa Bunge, Anne Makinda, jambo lililosababisha kutojadiliwa kwa hoja binafsi ya Mbunge wa Kawe, 

Halima Mdee (CHADEMA) iliyohusu kodi hiyo katika mkutano wa Bunge lililopita kwa kisingizio cha kukosekana kwa muda wa kufanya hivyo.

Hata hivyo, takwimu zilizotolewa na kampuni za simu zinaonyesha kuwa miongoni mwa wamiliki wa laini za simu milioni 22; milioni nane wanatumia chini ya sh 1,000 kwa mwezi.

Baada ya malalamiko hayo, Rais Kikwete alikutana na wadau wa mawasiliano ambao ni wamiliki wa kampuni za simu Tanzania (MOAT), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri wa Fedha, William Mgimwa, kisha kuwaagiza waiondoe kodi hiyo.

“Rais alisema lengo kuu la mkutano huo liwe kupendekeza jinsi ya kuziba pengo la sh bilioni 178 zitakazopotea katika bajeti iwapo kodi hiyo itafutwa.

“Alisema hawezi kuifuta moja kwa moja kodi hiyo, bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha kujazia pengo litakalotokeza huku tayari Bunge limezipangia matumizi,” alinukuliwa Makamba baada ya kikao hicho na rais.
Kwa upande wake, rais alikaririwa akiwaambia wadau hao wa mawasiliano kwamba: 

“Nakuombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tutajaza pengo hili la sh bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito, na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu.”

Licha ya agizo hilo la rais kutekelezwa kwa MOAT kutakiwa kuongeza kodi nyingine iitwayo ‘Excise duty’ kutoka asilimia 14 hadi 17 bila kujali kwamba katika Bunge la bajeti kodi hiyo iliongezwa kutoka asilimia 12 hadi asilimia 14, tozo hiyo ya laini za simu haijaondolewa.

Wachambuzi wa masuala ya siasa na mawasiliano walisema kutojadiliwa kwa mabadiliko ya kodi hiyo ya simu ni dalili kwamba Waziri wa Fedha amezidiwa nguvu na kiti cha spika kinachounga mkono hoja hiyo ya Chenge na kushindwa kutekeleza agizo la rais.

Wataalamu wa mawasiliano walilieleza gazeti hili kwamba kuongezeka kwa kodi hiyo kutaifanya Tanzania kuwa na kiwango cha juu cha kodi kuliko nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ushauri wa wataalamu hao ulibainisha kwamba kuongezeka kwa kodi hiyo kunaleta nafuu kidogo kuliko ile ya laini za simu inayomuumiza zaidi mwananchi wa kawaida.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate