KLABU ya Arsenal imemsaini Mesut Ozil kutoka Real Madrid kwa dau la rekodi katika klabu hiyo, Pauni Milioni 42.5.
Kiungo huyo amesaini Mkataba wa miaka
mitano kwa mshahara wa Pauni 140,000 kwa wiki, baada ya kukamilisha
vipimo vya afya nchini Ujerumani Jumatatu, licha ya Paris Saint-Germain
kutokea na ofa nzuri mapema siku hiyo ya mwisho ya usajili.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger aliwahi
kumtaka kiungo huyo miaka sita iliyopita, lakini Ozil, ambaye atavaa
jezi namba 11 Uwanja wa Emirates, sasa ameshawishika kumfuata Mjerumabi
mwenzake, Per Mertesacker na Wenger katika klabu hiyo.
Ozil alisaini Real Madrid kutoka Werder Bremen mwaka 2010 kwa ada ya Pauni Milioni 12.4.


Anafaa: Ozil amecheza mechi 158 Real katika miaka zaidi ya mitatu

Fanatic: Arsenal fans show their support for Ozil outside their training ground in London Colney.
No comments:
Post a Comment