
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha na Balozi wa Marekani nchini
Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Alfonso Lenhardt na mke wake siku ya jana
walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa
ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha ubalozi hapa nchini.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga
mke wa Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe
Alfonso Lenhardt siku ya jana walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na
serikali yake kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha ubalozi
hapa nchini. Mama Salma Kikwete alikuwepo pia katika kuwaaga
wanadiplomasia hawa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akimsindikiza Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake
Mhe Alfonso Lenhardt siku ya jana walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na
serikali yake kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha ubalozi
hapa nchini.
PICHA NA IKULU
Balozi wa Marekani amaliza muda wake hapa Nchini
Tanzania na Marekani zimeimarisha
mahusiano yao katika kipindi cha miaka minne iliyopita kutokana na
uhusiano na ushirikiano mzuri wa balozi anaemaliza muda wake nchini Mh.
Alfonso Lenhardt.
"Asante kwa kazi nzuri uliyoifanya
katika kipindi chote cha miaka minne uliyoitumikia hapa Tanzania. Mambo
mengi na makubwa yenye kuleta maendeleo na manufaa kwa Tanzania
yamefanyika hapa nchini na umeyasimamia na kuyafanikisha ipasavyo" .
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemueleza
Balozi Lenhardt siku ya jana alipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali
yake kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha ubalozi hapa
nchini.
Rais Kikwete amesema ushirikiano wa
nchi hizi mbili umekua na kuimarika zaidi na anatarajia kuwa balozi
ajaye naye atakuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza na kuimarisha
zaidi mahusiano baina ya nchi hizi.
Naye balozi Lenhart amesema Tanzania iko moyoni mwake na ataendelea kuwa balozi wa Tanzania popote alipo .
" Nikushukuru wewe mheshimiwa Rais na
serikali yako kwa ushirikiano mzuri na utayari wa kunisikiliza na
kunisaidia wakati wote nilipohitaji ushauri wako, umekuwa msaada mkubwa
kwangu. Asante kwa ushirikiano wako na siku zote nitaendelea kuwa balozi
wa Tanzania kwani Tanzania iko moyoni mwangu".
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
Dar es Salaam.
07 October, 2013
No comments:
Post a Comment