MRADI wa kusaidia watoto na wasiojiweza kupitia mpira wa miguu
(Football for Hope), mkoani Iringa, uliofadhiliwa na Shirikisho la Soka
la Kimataifa (FIFA), unatarajiwa kufunguliwa rasmi Oktoba 13 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar
Tenga, FIFA hutoa mradi huo kwa baadhi ya nchi kuzingatia mambo
mbalimbali ikiwemo utawala bora, kwa kupitia taasisi zisizo za
kiserikali (NGOs) ambapo kwa Tanzania umepatikana kupitia taasisi ya
Iringa Development of Youth, Disabled and Child Care (IDYDCC).
Tenga ameishukuru FIFA kwa msaada huo, kwani ni mkubwa na kuongeza
kuwa ni matumaini yake utatumika kwa lengo lililopangwa kwa kusaidia
watoto kielimu na wasiojiweza kwa kupitia soka.
Hata hivyo, Tenga alikiri kuwa mchakato huo haukupita moja kwa moja TFF.
Mradi huo utakuwa na jengo na sehemu ya watoto kucheza, ambapo umejengwa maeneo Mkimbizi, Mtwivila.
Aliongeza kuwa ni wastani wa nchi 13 duniani kwa mwaka zinapata mradi
huo kutoka FIFA, jambo ambalo linachangiwa pia na uhusiano, ushirikiano
uliopo kati ya Tanzania na shirikisho hilo.
No comments:
Post a Comment