FINALI ya shindano la kuimba la Epiq BSS 2013 inatarajiwa kurindima jijini Dar es Salaam Novemba 16.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Jaji
Mkuu wa shindano hilo, Ritha Poulsen, alisema shindano hilo limefikia
patamu sasa, ambapo washiriki 12 wamesalia katika kinyang’anyiro hicho.
Alisema kwa sasa mchakato wa Watanzania kuanza kupiga kura unaanza,
ambapo mtumaji atatuma ujumbe mfupi akianza na neno kura, kisha namba ya
mshiriki, kwenda namba 15530.
Aliongeza kuwa washiriki hao 12 wamebaki baada ya mchujo na wawili wamepatikana kupitia njia ya simu kwa kutuma sauti.
Washiriki hao ni Amina Chibaba, Elizabeth Mwakijambile, Emmanuel
Msuya, First Godfrey, Francis Flavian, Furaha Charles, Furaha Mkwama,
Joshua Kahoza, Maina Thadei, Mandela Nicholas, Melisa John na Raymond
John.
Naye Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, ambao ndio wadhamini wakuu, Sajid
Khan, aliwataka wananchi wawapigie kura washiriki wanaoamini ni wazuri
na watafanya vema katika soko la muziki hapa nchini.
Mshindi wa Epiq BSS mwaka huu, anatarajiwa kujinyakulia kitita cha sh
milioni 50. Mshindi wa mwaka jana aliibuka Walter Chilambo.
No comments:
Post a Comment