FUNDI wa kuchomelea vyuma, Ngas Matawa (35), mkazi wa Temeke, amefariki dunia juzi kwa kunaswa na umeme.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime, alisema jana kuwa
fundi huyo alikutwa na mkasa huo wakati akiendelea na kazi ya kuchomelea
bodi ya gari aina ya Scania, huku akiwa amejifunika bati kwa ajili ya
kujikinga na mvua, lakini kwa bahati mbaya bati liligusa bodi ya gari
ambayo ilikuwa imeunganishwa na umeme na kusababisha Matawa kunaswa na
umeme.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke na upelelezi unaendelea.
Katika tukio jingine, Vililia Mkeka (47), mkazi wa Mbezi Beach A, amekutwa amefariki dunia chumbani kwake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema
juzi, saa 4:00 asubuhi Mkeka alikutwa amekufa chumbani kwake huku mwili
wake ukiwa umeharibika vibaya na hauna jeraha lolote.
Wambura alisema baada ya maiti kufanyiwa uchunguzi iligundulika kuwa chanzo cha kifo chake ni kuugua malaria.
No comments:
Post a Comment