MAMA Lishe, Husnut Anthony John, ameibuka mshindi wa nyumba ya
kisasa iliyoko Kigamboni jijini Dar es Salaam katika droo ya mwisho ya
Promosheni ya Airtel Yatosha.
Akizungumza wakati wa promosheni hiyo jijini Dar es Salaam juzi,
Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga, alisema mshindi huyo ni wa mwisho
katika promosheni ya nyumba.
Aliwashukuru wateja walioshiriki na walioshinda huku akiwataka wateja
wote kuendelea kufurahia huduma ya Airtel yenye vifurushi vya bei nafuu.
Akizungumzia ushindi wake, Mama Lishe huyo alisema hakutarajia kama angeshinda katika promosheni hiyo.
Airtel Yatosha Shinda Nyumba, ilizinduliwa Julai 5, mwaka huu na kudumu kwa siku 90.
Wakati wa promosheni hiyo, Airtel imetumia zaidi ya sh milioni 410 kwa zawadi za washindi mbalimbali.
Naye Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando, alisema huduma ya
vifurushi vya Airtel Yatosha bado vinaendelea kuboreshwa, hivyo wateja
waendelee kuvifurahia.
No comments:
Post a Comment