Watoto hao walikuwa wakitafuta vyuma hivyo katika eneo la makazi ya zamani wanajeshi, msemaji wa Jeshi ameiambia BBC.
Mwandishi wa Habari wa BBC James
Copnall amesema baruti ambazo hazijalipuka kwenye migodi bado ni tatizo
kubwa Sudan Kusini kufuatia miongo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kuna operesheni maalum ya kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Sudan Kusini, lakini milipuko imekuwa ikiua watu kila mwaka.
Watoto wenye umri kati ya miaka 10 na 14
wameuawa katika eneo la makazi ya wanajeshi ya zamani katika wilaya ya
Souk Sita katika mji wa Juba, msemaji wa Jeshi Kanali Philip Aguer
amesema.
Amesema raia wa Uganda aliyekuwa pamoja watoto hao akitarajia kununua vyuma hivyo chakavu naye amejeruhiwa.
Sudan Kusini ilipata uhuru mwaka 2011 baada ya
muda mrefu wa migogoro na Sudan na kubakia miongoni mwa mataifa maskini
sana duniani.
No comments:
Post a Comment