Viongozi
wa matawi mbali mbali ya Young Africans jijini Dar es salaam pamoja na
Baraza la Wazee wa klabu kwa pamoja leo wameahidi ushindi mnono siku ya
jumapili katika mchezo wa jumapili dhidi ya watani wa Jadi Simba SC
katika uwanja wa Taifa.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, katibu wa
baraza la wazee wa klabu ya Yanga Ibrahim Akilimali amesema wanashukuru
viongozi kazi zao wamemaliza, makocha na wachezaji pia wamemaliza na
sasa wao wanamalizia kazi ili kunogesha ushindi huo.
"Yanga tuna
tamaduni zetu, sehemu yoyote ile ina asili yake, hivyo kwa hivi sasa
sisi wazee kwa pamoja tunaahidi lazima tumchinje mnyama siku ya
jumapili, uwezo na nia tunao hivyo washabiki wa Yanga mje kwa wingi
uwanja Taifa kuishangilia timu yao" alisema Akilimali.
Aidha
Akilimali alisema kwa hivi sasa hawana wasi wasi na kikosi chao, watani
wetu wanaweweseka kuona speed yetu ni yali ya juu, tunachoomba ni
waamuzi kuchezesha soka kwa kufuata kanuni 17 za mchezo na kama
watafanya hivyo basi lazima tumchape mnayma siku ya jumapili.
Naye
kiongozi wa tawi la Temeke Kati Bakili Makele akiongea kwa niaba ya
viongozi wa matawi, alisema msimu huu Yanga imejipanga vizuri na wana
uhakika wa kupata ushindi siku ya jumapili kutokana na kuwa na kikosi
bora.
Sisi hatutaki magoli ya kupewa kama wenzetu, mechi zote
wanapewa penati, sisi tunataka kushinda ki halali kwa kufuata sheria 17
za soka, tunaamini kwa jinisi tulivyojiandaa na hali inayoendelea kwa
kufuata mila na desturi ni lazima mnyama achinjwe siku ya jumapili.
Kikosi
cha Young Africans kinaendelea na mazoezi kisiwani Pemba kujiandaa na
mchezo wa siku ya jumapili dhidi ya Simba SC ambapo mpaka baada ya
mazoezi ya leo hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja na wote wako fit kwa
ajili ya mchezo.
No comments:
Post a Comment