MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga jana waliendeleza wimbi la
ushindi baada ya kuichapa Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani, Morogoro
kwa mabao 2-0.
...dakika sita tu kuanza kucheza na
nyavu kwa bao la Mrisho Ngasa
Kwa matokeo hayo, Yanga wamefikisha pointi 12 baada ya kushuka dimbani
mara saba na kuchupa hadi nafasi ya pili nyuma ya watani zao Simba
wenye pointi 15.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyopigwa Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam,
Yanga iliwachukua dakika sita tu kuanza kucheza na
nyavu kwa bao la Mrisho Ngasa akimalizia pasi safi ya Mrundi Didier
Kavumbagu.
Kama haitoshi, dakika ya 20, Kavumbagu naye alimsalimia kipa wa Mtibwa
Sugar, Hussein Sharrif kwa kupachika bao la pili akiitumia pasi ya
Ngasa.
Mtibwa walijibu mapigo, lakini Vicent Barnabas alishindwa kuitendea
haki pasi ya Ally Shomari dakika ya 23, wakati alipopiga nje mpira kwa
kichwa, kabla ya dakika ya 33, Ngasa kubaki na Kipa Sharrif lakini shuti
lake jepesi likadakwa.
Hadi mwamuzi Isihaka Shirikisho anapuliza filimbi kuashiria mapumziko matokeo yalikuwa 2-0.
Kipindi cha pili, Mtibwa ilizinduka hasa baada ya kufanya mabadiliko kadhaa, lakini bahati haikuwa yao.
Awali kabla ya kuanza kwa mchezo, Yanga walizuia Azam TV kurusha mechi
yao hiyo ya nyumbani kwa madai kuwa mazungumzo bado yanaendelea.
Azam TV walirejesha kamera zao dakika ya 40 na kuendelea na kazi, baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuingilia.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema walilazimika kuingilia
kati, kwani suala hilo ni la kimkataba, hivyo mechi kuonyeshwa ni mali
ya shirikisho hilo na Azam TV, wala sio klabu.
Yanga: Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite/Juma Abdul, David Luhende,
Nadir Haroub ‘Canavaro’, Kelvin Yondani, Athumani Idd ‘Chuji’, Simon
Msuva/Nizar Khalfan, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Mrisho Ngasa, Hamis
Kiiza/Said Bahanuzi.
Mtibwa: Hussein Sharrif, Hassan Ramadhani, Paulo Ngalema, Salvatory
Ntebe/Dickson Daudi, Salim Abdallah, Shabani Nditi, Ally Shomari, Awadh
Juma, Mussa Hassan ‘Mgosi’, Shabani Kisiga, Vicent Barnabas/Masoud
Mohamed.





No comments:
Post a Comment