Kwa miaka mingi wanafunzi
wa hapa nchini wamekuwa wakitumia vitabu vya watunzi mbalimbali
ulimwenguni kama vile, The river between, Song of Lawino na vinginevyo
hatimaye Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of
Tanganyika, IST) imekiingiza kwenye mtaala wake wa kiswahili, kitabu cha
mtunzi mahiri wa riwaya hapa nchini, Eric James Shigongo kiitwacho kifo
ni haki yangu.
Akizungumza na gazeti hili shuleni hapo hivi karibuni, Mwalimu wa
somo la Kiswahili katika shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Madam
Hilda, alisema shule yake imeamua kutumia kitabu hicho kwenye mtaala
wake baada ya kamati ya shule hiyo kukipitia kiundani na kubaini ubora
wa hadithi zake zinazokwenda na wakati tuliopo pamoja na matumizi sanifu
ya lugha ikiwemo mambo mengi ya kujifunza.
Hilda alisema baada ya kuona umuhimu uliopo kwenye kitabu hicho
shuleni hapo shule iliamua kumuita mtunzi huyo ambaye walimu na
wanafunzi walikuwa na shauku ya kumuona ‘live’ badala ya kusoma riwaya
zake kwenye vitabu.
Kufuatia wito huo, Shigongo alifika chuoni hapo
na kukutana na wanafunzi wa shule hiyo ambao walimuuliza maswali
mbalimbali yaliyokuwa yakiwatatiza kwenye riwaya.
Wanafunzio hao walimuomba Shigongo awafundishe mambo kadhaa kwenye
utunzi wa riwaya ambapo walionekana kuyafurahia majibu waliyopewa ambayo
yalionekana kuwaingia vyema akilini.
Baada ya kuwafundisha mambo mbalimbali wanafunzi hao walimshukuru
Shigongo kwa kuwapa baraka za kutumia kitabu chake kwenye masomo yao na
kuwapa fursa ya kuwapa ushauri muda wowote ambao watauhitaji.
Kufuatia wanafunzi hao kutumia kitabu hicho mitihani mbalimbali ya
wanafunzi hao ikitoka kwenye kitabu hicho hivyo wanafunzi hao wanatakiwa
kukichimba zaidi kitabu hicho.
Mbali na riwanya hiyo Shigongo aliwatafadhalisha wanafunzi hao
kutobweteka na kutumia nguvu za wazazi wao kwani hawajui ya kesho na
keshokutwa.
Aliwashauri wanafunzi hao kutokuwa kama wazazi wao kimaisha na kuwa
zaidi ya wazazi wao yaani kama baba alikuwa mkuu wa wilaya mtoto
anatakiwa kuwa waziri na kama baba alijenga ghorofa moja mtoto anatakiwa
kuwa zaidi.
CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment