Stori: Mbeya Yetu
NDUGU wa watuhumiwa wawili kati ya wanne waliohukumiwa kunyongwa hadi
kufa baada ya kupatikana hatia la kumuua aliyekuwa Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, John Mwankenja waliangua vilio baada ya
hukumu hiyo.
Marehemu John Mwankenja, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe enzi za uhai wake.
Jumatano iliyopita, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya aliyekuwa
ikiendesha vikao vya kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Rungwe, Samuel
Karua alipotoa hukumu hiyo, baadhi ya ndugu wa waliohukumiwa walilipuka
kwa vilio kutokana na uchungu wa adhabu hiyo.
Hukumu ya kesi hiyo iliahirishwa kutolewa zaidi ya mara tatu na kuzua
hali ya sintofahamu kwa ndugu wa washtakiwa na wafuatiliaji wa kesi
hiyo, wengi wakihoji kulikoni!
Kabla ya kusoma kwa hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali,
Archiles Mulisa aliwataja watuhumiwa wote wanne kuwa ni Hakimu
Mwakalinga, Daudi Mwasipasa, Obote Mwanyingili na Kelvin Myovela
wanaokabiliwa na tuhuma za kumuua kwa makusudi John Mwankenja.
Baadhi ya wananchi wakiwa nje ya mahakama. |
Alisema watuhumiwa hao wenye kesi namba 131/2012 walitenda kosa hilo
Mei 19, 2011 katika Kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira, Wilaya ya
Rungwe mkoani Mbeya.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Karua ambaye alianza majira ya saa 8:37
mchana na kumaliza saa 9:37 alasiri alisema katika kesi hiyo upande wa
mashtaka na utetezi haubishani kuhusu kifo cha marehemu.
Aliongeza kuwa pande hizo pia hazibishani kuhusu ripoti za kitaalam
na dhamira za mauaji hayo bali kinachobishaniwa ni uhusika wa watuhumiwa
hao dhidi ya mauaji hayo.
Alisema katika kutetea hoja zao upande wa mashtaka ulipeleka
mahakamani mashahidi 11 wakiongozwa na shahidi namba moja aliyewatuhumu
washtakiwa kuhusika na tukio hilo.
Shahidi huyo namba moja Weston Jacob (17) mkazi wa Kiwira na
mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Kipoke ambaye
pia ni mjomba wa marehemu ambaye aliiambia mahakama kuwa siku ya tukio
akiwa nyumbani saa 2: 30 usiku marehemu alifika na kupiga honi ya gari
akitaka afunguliwe mlango.
Kutokana na ushahidi huo, Jaji Karua alisema mshtakiwa namba moja na
namba mbili ambao ni Hakimu Mwakalinga na Daudi Mwasipasa wanatiwa
hatiani kuhusika moja kwa moja na mauaji kutokana na kukiri kwao kwa
mlinzi wa amani, mchukua maelezo na vipimo vya vinasaba.
Alisema mshtakiwa namba tatu, Obote Mwanyingili yeye anatiwa hatiani
kutokana na kosa la kumhifadhi mtuhumiwa namba moja baada ya kutoka
kufanya mauaji hivyo yeye hausiki na kosa hilo.
Jaji Karua alisema mshtakiwa namba nne, Kelvin Myovela anatiwa hatiani kutokana na kuhifadhi silaha iliyotumika katika mauaji hayo ingawa hakuhusika na kitendo hicho.
Jaji Karua alisema mshtakiwa namba nne, Kelvin Myovela anatiwa hatiani kutokana na kuhifadhi silaha iliyotumika katika mauaji hayo ingawa hakuhusika na kitendo hicho.
Kutokana na ushahidi huo, Jaji Karua alisema washtakiwa namba moja na namba mbili wanahukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Aliongeza kuwa, mshtakiwa namba tatu aliyemhifadhi mtuhumiwa wa kwanza ataenda jela miaka saba, mshtakiwa namba nne, Kelvin Myovela aliyehifadhi silaha iliyotumika kwenye mauaji hayo atatumikia kifungo cha miaka saba.
Aliongeza kuwa, mshtakiwa namba tatu aliyemhifadhi mtuhumiwa wa kwanza ataenda jela miaka saba, mshtakiwa namba nne, Kelvin Myovela aliyehifadhi silaha iliyotumika kwenye mauaji hayo atatumikia kifungo cha miaka saba.
No comments:
Post a Comment