Stori: Mashaka Baltazar,Mwanza
TUKIO la Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza, Henry Matata, kunusurika mkong’oto kutoka kwa madiwani wa manispaa hiyo wakidai kutomtambua lilikuwa kama sinema.
TUKIO la Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza, Henry Matata, kunusurika mkong’oto kutoka kwa madiwani wa manispaa hiyo wakidai kutomtambua lilikuwa kama sinema.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri juzi
(Alhamisi) asubuhi baada ya meya huyo kufungua kikao cha Baraza la
Madiwani wa Manispaa ya Ilemela.
Katika kikao hicho, madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) walimtaka meya huyo aondoke kwenye kiti wakidai kutomtambua
ndipo ukaibuka mtiti wa mshikemshike nguo kuchanika.
Huku vita ya
maneno ikiendelea, Matata aliwaamuru madiwani hao watoke nje ya ukumbi
lakini wakamvimbia wakimtaka yeye ndiye atoke.
Baada ya kadhia hiyo kuwa kubwa huku madiwani hao wakisukumana wao
kwa wao wakitaka kumpiga meja huyo, ndipo simu ikapigwa polisi Kirumba
ili waje kutuliza hali ya hewa.
Hata hivyo, wakati askari hao wakisubiriwa ndipo vijana wenye miili mikubwa ‘mabaunsa’ waliodaiwa kuwa wapambe wa
Hata hivyo, wakati askari hao wakisubiriwa ndipo vijana wenye miili mikubwa ‘mabaunsa’ waliodaiwa kuwa wapambe wa
Matata wakavamia ukumbini kumnusuru na hakuna mtu aliyekamtwa wala kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, ilikuwa ni sinema ya bure huku mabaunsa wakipongezwa kwa namna walivyomuokoa meya huyo kimafia.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, ilikuwa ni sinema ya bure huku mabaunsa wakipongezwa kwa namna walivyomuokoa meya huyo kimafia.
“Kweli kabisa mabausa wamefanya kazi nzuri kwa sababu hali ilikuwa
mbaya sana. Kama siyo kumuondoa kimafia na kiintelijensia,
wangemalizana,” alisema Antony Maduhu aliyeshuhudia kila kitu.CREDIT GPL
No comments:
Post a Comment